Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akizundua ofisi mpya ya ndege ya ATCL Jijini Arusha |
Mkuu wa Mkoa wa Arusha akipata maelezo ya namna wafanyakazi wa ATCL watafanyakazi katika ofisi ya Arusha |
Na Ahmed Mahmoud Arusha
Watanzania
wametakiwa kupenda na kutangaza vitu mbali mbali ambavyo vinazalishwa
hapa nchini kwa lengo la kusaidia kuonyesha Uzalendo kwa Taifa.
Akizungumza
kwenye uzinduzi wa Ofisi ya shirika la Ndege la Tanzania ATCL Mkuu wa
mkoa wa Arusha Mrisho Gambo kwenye hafla iliofanyika kwenye Jengo la
Mafao house jijini Arusha alisema kuwa Uzalendo ni jambo jema na
linahitaji Sana kwa watanzania kuitangaza shirika hilo na kuliunga
mkono.
Alisema kujivunia
uwepo wa shirika hilo ambalo linaitangaza Tanzania kote linapoenda
sanjari na kuongeza watalii wanaokuja kuitembelea nchi yetu hivyo
kuongeza pato la taifa.
Aliipongeza
Bodi ya wakurugenzi wa shirika la Ndege kwa kazi nzuri ya kuendelea
kuliboresha shirika hilo na kuwaomba watanzania kulipenda na kujivunia
shirika hilo.
Awali
akimkaribisha mgeni rasmi Mkuu wa mkoa wa Arusha mwenyekiti wa Bodi ya
wakurugenzi wa shirika hilo mhandisi Emmanuel Koroso alisema kuwa
shirika limejipanga kuhakikisha linaenda na hadhi ya shirika la Ndege
nchini ndio maana wakafungua ofisi hizo zinazoendana na hadhi ya shirika
hilo.
Alisema shirika
hilo limeamua kuendana na mageuzi makubwa ya kiundeshaji kuendana na
kuhakikisha shirika hilo linaenda na malengo na matarajio ya serikali ya
awamu ya tano chini ya Dkt.John Magufuli kuwa shirika Bora lenye
kuchangia kukuza uchumi wa watanzania.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa shirika hilo Ladslaus Matindi alisema ofisi
hiyo itahudumia na kusimamia pia Ofisi za mkoa wa Kilimanjaro ambapo
aliwataka watanzania kutumia usafiri huo kwa sasà wanafika katika mikoa
10 nchini lengo likiwa kufikia mikoa yote.