Kem
Senou Pavel Daryl, ni kijana raia wa Cameroon aliyepatwa na ugonjwa wa
homa kali inayosababishwa na virusi vya Corona, alithibitika kupona
baada ya kutengwa kwa ajili ya uangalizi maalumu kwa siku 14.
Daryly
mwenye umri wa miaka 21 ambaye ni mwanafunzi raia wa Cameroon anayeishi
katika mji wa Jingzhou, amesema kuwa hata baada ya kugundulika kupata
maambukizi hayo, hakuwa na mpango wa kuondoka China, hata kama Serikali
ya Cameroon ingeshinikiza kuwa hivyo.
Akiwa
katika chumba chake cha kupatiwa matibabu alichotengwa kwa siku 14,
kijana huyo alisema “Chochote kitakachofanyika sitaki kupeleka ugonjwa
Afrika”.
Alikuwa
anaugua homa kali, kukohoa vibaya na kuonesha dalili za mafua,
alitibiwa kwa antibiotiki na dawa za kutibu wagonjwa walio na virusi vya
Ukimwi na baada ya wiki mbili ya uangalizi alianza kuonesha dalili ya
kupona.
Uchunguzi
wa kimatibabu wa CT scan haukuonesha dalili zozote za ugonjwa na kwamba
alikuwa mtu wa kwanza mwenye asili ya Kiafrika aliyepona baada ya
kuambukizwa na virusi hatari vya corona na Serikali ya China iligharamia
matibabu yake.
Credit: BBC