Makombora
manne leo hii yamevurumishwa karibu na ubalozi wa Marekani mjini
Baghdad na kambi ya kijeshi ambayo inatumiwa na vikosi vya Marekani
ndani la Ukanda wa Kijani.
Hata
hivyo hakuna athari kubwa zilizoripotiwa. Msemaji wa operesheni ya
kijeshi ya Marekani nchini Iraq, Kanali Myles B. Caggins, amesema
mashambulizi hayo yalitokea majira ya tisa na nusu Alfajiri, na kuongeza
kuwa yalipiga tu kambi inayohifadhi wanajeshi wa Marekani na wa
muungano.
Hata
hivyo maafisa watatu wa usalama wa Iraq wamesema mawili kati ya
makombora hayo yaliangukia katika eneo la ubalozi wa Marekani, wakati
lingine likitua katika kambi ya jeshi la muungano.
Maafisa
hao wa Iraq waliyasema hayo kwa masharti ya kutotajwa majina kwa kuwa
hawana mamlaka ya kuzungumza na vyombo vya habari.