CCM HAKINA BEI YA BINADAMU BALI UTUMISHI KWA WANANCHI:MASAWE

Kamati ya siasa wilaya ya Arusha mjini ukiendelea na kikao chake pamoja na kuwapokea waliokuwa  madiwani wa kata za Ngarenaro na Sakina waliojiunga na chama hicho leo

Viongozi wa ccm kata ya Ngarenaro waliomsindikiza aliyekuwa Diwani wa kata hiyo Isaya Doita kujiunga na chama hicho leo jijini Arusha picha zote na Ahmed Mahmoud Arusha

Wajaumbe wa kamati ya siasa CCM ya  halmashauri ya Jiji la Arusha kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa UWT wilaya hiyo Merry Kisaka Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Ally Meku Issa Saidi Omary wakifuatilia maelezo ya Mwenyekiti wao Joseph Masawe hayupo pichani kwenye kikao chao pia kuwapokea madiwani wapya wawili kutoka chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA)ISAYA DOITA na DAMUNI MELAMALI wa kata za  Ngarenaro na Sakina leo jijini Arusha picha zote na Ahmed Mahmoud Arusha

Pichani katikati Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Arusha Mjini Joseph Masawe akiwa na Katibu wake Mwita Zakaria pamoja na Katibu Mwenezi wa CCM wilaya wakifuatilia maelezo ya madiwani hao mbele ya kamati ya siasa wilaya hiyo leo jijini Arusha 


Pichani wa kwanza ni Damuni Melamali aliyekuwa Diwani wa kata ya Sakina na aliyekuwa Diwani wa kata ya Ngarenaro Isaya Doita wakifuatilia hotuba ya Mwenyekiti wa CCM wilaya wakati akiwakaribisha kwenye chama hicho leo jijini Arusha

Juu na chini ni picha ya pamoja ya viongozi wa kamati ya siasa ya wilaya pamoja na viongozi wa chama hicho wa kata za Ngarenaro na Sakina baada ya kuwapokea madiwani hao wastaafu ndani ya chama hicho wakiongozwa na Mwenyekiti wa CCM wilaya Joseph Masawe picha zote na Ahmed Mahmoud Arusha.

Chama cha Mapinduzi CCM wilaya ya Arusha kimewapokea madiwani wawili wa chama cha demokrasia na maendeleo Chadema walijiunga na chama hicho kuunga Juhudi za mh.Rais na Mwenyekiti wa chama hicho Dkt John Magufuli.

Akiongea Mara baada ya kuwapokea ndani ya chama hicho Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Arusha mjini Joseph Masawe amesema kuwa hakuna bei ya kumunua binadamu bali bali kila moja anatumia demokrasia ya kuamua sehemu anayoona inafaa kuweza kutekeleza haki yake ya kikatiba ikiwemo kutumia mawazo yake na akili kujiunga na vyama vya kisiasa ikiwemo CCM .

Ameeleza kuwa chama hicho hakijawahi kufikiria kununua watu bali kimejipanga kuahughulika na shida za wananchi ndio maana wenye ufahamu wanaona ndio sehemu sahihi ya kufanyakazi za kuwatumikia wananchi kuwaletea maendeleo.

"Chama chetu hakijui bei ya kumunua mtu hivyo wanaojiunga na Cha hichi wanafuata mazuri ya ndani ya CCM ikiwemo kazi nzuri ya Mwenyekiti wetu taifa na Rais Dkt.John Magufuli sio vingine ni kuunga kuonyesha Juhudi za Rais katika kuwatumikia watanzania"

Kwa upande wake Katibu wa ccm wilaya  chama Mwita Zakaria  amesema kuwa chama hicho hadi Sasa teyari kimewapokea waliokuwa madiwani kwenye halmashauri ya jiji la Arusha 12 ikiwemo hao wawili

Ameeleza kuwa Cha hicho kimeanda utaratibu wa kuwapokea kwenye kata zao hapo baadae kwa kuwa sasa Kuna Ugonjwa wa Covid 19 au virusi vya Corona nao wanaheshimu maelekezo ya Serikali kutokuwa na mikusanyiko isiyo ya lazima ndio maana wakaamua kufanya mapokezi hayo na kamati ya siasa ya wilaya.

*Chama chetu kina wanachama lukuki hawa isingekuwa Ugonjwa wa Covid 19 ambao maelekezo ya Serikali yanatutaka tusifanye mikusanyiko isiyo ya lazima tungefanya mikutano kwenye kata zao kuwapokea kwa kuwa tunao wanachama lukuki ndani ya kata hizo"

Nae Isaya Doita alisema kuwa anashukuru kwa mapokezi hayo na kuahidi ushirikiano wa hali ya juu kuhakikisha chama hicho kinarudisha Jimbo la Arusha mikononi mwa CCM wakati ukifika

Alisema wanaodhani amenunuliwa wafute dhana hiyo kwani kwa mwenye akili haambiwi tazama anaona matukio yanayoendelea ndani ya chama katika kushughulikia shida za wananchi kama ilani CCM inavyoelekeza .

Awali akiongea Damuni Melimali alisema kuwa msingi wa chama hicho ni mkubwa ndio maana akaamua kujiunga na CCM kuunga mkono Juhudi za Serikali ya awamu ya tano chini ya Dkt.John Magufuli kwa utumishi uliotukuka unaojali wanyonge ndio maana akaamua kwa dhati yake bila ushawishi kujinga kushirikiana nae kujenga taifa hili.

Mwenyekiti wa ccm wilaya Joseph Masawe akiongoza kamati ya siasa kupokea kamati ya siasa wilaya hiyo kuwapokea waliokuwa madiwani wa kata za Ngarenaro na Sakina waliojiunga na chama hicho leo jijini Arusha.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post