RC WA KIGOMA AKATAZA WATOTO KUFANYABIASHARA


Mkuu wa Mkoa wa kigoma brigedia mstaafu Emanuel Maganga(wakatikati)akiongea na wafanyabiashara wa dagaa katika soko la mwalo wa kibirizi wakati wa ziara yake ya kukagua utekelezaji wa agizo la serikali kwa wananchi kujilinda dhidi ya virus vya corona

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia mstaafu Emanuel Maganga akinawa mikono na maji tiririka kwaajili ya kujikinga na virusi vya corona wakati akiingia katika hotel ya green view kufanya  ukaguzi wa utekelezaji wa agizo la serikali juu ya kujilinda na virusi vya corona



Na Editha Karlo,Kigoma
MKUU wa mkoa Kigoma Emanuel Maganga amepiga marufuku wanafunzi na watoto kutumika kufanyabiashara  kwenye masoko na kuona  watakao kiuka  agizo hilo.

Akizungumza leo wakati akifanya Ziara kwenye masoko ya Buzebazeba Ujiji, Mwanga na Kibirizi kukagua utekelezaji wa agizo la serikali kujilinda dhidi ya virus vya Corona alisema kuwa watoto watakaokuwepo wakiuza kwenye masoko wazazi wao watachukuliwa hatua.

Alisema kuwa serikali ilikuwa na maana kubwa kufunga shule na vyuo ili kukiweka tayari kwa ajili ya kudhibiti ugonjwa huo hivyo serikali haitakubali kuona wazazi na walezi wakiwatumia watoto hao kinyume na maagizo ya serikali.

Mkuu huyo wa mkoa amewataka wafanyabiashara kutoa maelekezo kwa wateja wao kuingia mmoja mmoja kununua bidhaa na kuepusha msongamano ili kujikinga na Virus vya Corona.

Akikagua vifaa vya kunawia mikono na dawa za kuua wadudu  (Sanitizer)  alitaka uongozi wa masoko na wafanyabiashara kuhakikisha kunakuwepo na vifaa vya kutosha na vinatumiwa na watu wote wanaoingia kwenye masoko hayo.

Awali akitoa tàarifa kwa Mkuu was mkoa Kigoma wakati wa Ziara hiyo Mwenyekiti wa wafanyabiashara wa soko la Buzebazeba, Amrani Abdul alisema walichangisha wafanyabiashara na kununua ndoo 17 na dawa kwa ajili ya kunawa mikono Ingawa kumekuwa na mwitikio mdogo kwa wafanyabiashara kuchangia kwa ajili ya ununuzi wa ndoo.

Alisema kuwa hata hivyo wametoa agizo kwa wafanyabiashara kuweka ndoo kila mmoja kwenye eneo lake la biashara na kwamba asiyetekeleza Hilo watatoa tàarifa kwa afisa afya ili wachukuliwe hatua.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji, Mwailwa Pangani alimweleza Mkuu we mkoa kwamba halmashauri imechukua hatua mbalimbali za kukabiliana na virus vya Corona iwapo vitaingia sambamba na uwepo wa maeneo maalum ya kuhifadhia watu watakaobainika kuwa na dalili za virus vya Corona

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post