Rwanda
imethibitisha visa 10 vipya vya maambukizi ya ugonjwa wa Corona siku
ya Jumapili na kufikisha 70 jumla ya watu wanaougua corona, Wizara ya
afya Rwanda imetangaza.
Katika
hotuba yake kwa taifa usiku wa Ijumaa Rais Paul Kagame alisema idadi
hiyo itaendelea kuongezeka kwasababu wale waliotangamana na waathirika
wanaendelea kutafutwa.
Katika
visa vya hivi punde vya maambukizi, watu sita walitokea Dubai, wawili
kutoka Afrika Kusini, mmoja kutoka Nigeria na mwigine alikuwa amesafiri
maeneo ya Afrika mashariki hivi karibunii, ilisema taarifa ya wizara ya
afya nchini humo.
Rwanda
inaongoza kwa visa vya maambukizi ya ugonjwa wa corona katika kanda ya
Afrika Mashariki ikiiwa na wagonjwa 70, ikifuatiwa na Kenya 42, Uganda
33, Tanzania 14, huku Burundi na Sudan Kusini zikiwa hazijarekodi visa
vyovyote vya maambukizi.