Waziri mkuu Kassim Majaliwa wa pili kushoto akiwa na mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Qwihaya Leonard Mahenda wa kwanza kushoto alipotembelea kiwanda chake cha nguzo Maginga
.........................................
WANAHANGA 801 wa Mafuriko wakazi wa kitongoji cha Mbingama kijiji cha Isele tarafa ya Pawaga wilaya ya Iringa wamepatiwa msaada wa zaidi ya shilingi Milioni 21.
toka kampuni ya Qwihaya General Enterprises ya mkoani Iringa .mwandishi Francis Godwin anaripoti kutoka Iringa
.........................................
WANAHANGA 801 wa Mafuriko wakazi wa kitongoji cha Mbingama kijiji cha Isele tarafa ya Pawaga wilaya ya Iringa wamepatiwa msaada wa zaidi ya shilingi Milioni 21.
toka kampuni ya Qwihaya General Enterprises ya mkoani Iringa .mwandishi Francis Godwin anaripoti kutoka Iringa
Akizungumza kwa niaba ya mkurugenzi wa kampuni hiyo meneja wa kampuni hiyo ya Qwihaya General Enterprises Leonard Mahenda ,meneja wake ambae alipeleka msaada huo kijijini kwa wanahanga Ntimbwa Mjema alisema kwa kupitia sera yao ya kurudisha sehemu ya faida wanayopata kwa wananchi, kampuni yao imeguswa na tukio la mafuriko lilowakumba wananchi hao ili nao waweze kuendelea kuishi maisha ya furaha zaidi .
“Baada ya kuwasiliana na mkuu wa wilaya na kuelezwa mahitaji ya wahanga hao, kampuni yetu kwa upande wake iliamua kutoa msaada wa roli tatu za nguzo hizi za ujenzi zenye thamani ya zaidi ya Sh Milioni 21 pamoja na mifuko 30 ya unga ya kilo 25 kila mmoja,” alisema.
Meneja huyo alisema kwa kupitia sera yao ya kurudisha sehemu ya faida yao kwa wananchi, kampuni yao itaendelea kutoa misaada ya aina hiyo na mingine muhimu kwa wananchi ili kuharakisha maendeleo yao mbali ya kutoa msaada huo kwa wahanga hao alisema wamekuwa wakitoa misaada mbali mbali pale inapohitajika kufanya hivyo.
Wahanga wa mafuriko hayo mbali ya kushukuru kwa msaada huo mirunda kwa ajili ya ujenzi wa nyumba zao za muda bado waliomba wadau wengine wajitokeze kuwasaidia kupata bati kwa ajili ya kuezekea na vifaa vingine vitakavyowawezesha kukamilisha ujenzi wa nyumba hizo za muda alisema John Msemwa kwa niaba ya wenzake .
Kuwa wameridhia uamuzi wa serikali wa kuwahamisha moja kwa moja kutoka katika kitongoji chao kilichokumbwa na mafuriko hayo na kwamba watageuza eneo hilo kuwa sehemu ya mashamba yao ili kujiinua kiuchumi japo kutokana na kupoteza mali zote uwezo wa kupata fedha za kununua bati na kuanza makazi ya kudumu kwa sasa ni mgumu kwao .
Akizungumza kwa niaba ya ya mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Iringa, Afisa Elimu Msingi Peter Fusi alisema pamoja na serikali kuendelea kushirikiana na wadau kurejesha katika hali ya kawaida maisha ya wahanga hao, tahadhari za kujikinga na janga la virusi vyacorona linatakiwa kuendelea kuzingatiwa.
Kuwa msaada huo ni mkubwa na serikali ya wilaya imefarijika kuona kampuni hiyo ya kizalendo ikiwa ni kampuni ya kwanza ndani ya mkoa huo kujitolea kwa kiasi kikubwa kuanza kuwasaidia wahanga hao wa mafuriko ambao wanahitaji misaada mbali mbali kutokana na kukumbwa na janga kubwa ya mali zao zote kusombwa na mafuriko .
Aktoa pongezi hiyo mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela katika tukio hilo la mafuriko yalisababisha kaya 218 zenye jumla ya wananchi 801 kuachwa bila makazi pia mali zao zote kikiwemo chakula chao cha akiba ni miongoni mwa vitu vilivyo athiriwa na mafuriko hayo yaliyotokea mapema mwezi huu .
Aidha alisema msaada huo wa mirunda kwa ajili ya kujengea nyumba za muda za kuishi wahanga hao wa mafuriko iliyotolewa na kampuni hiyo ya Qwihaya General Enterprises itawawezesha wahanga hao waliohamishwa toka katika kitongoji hicho kutumia msaada huo kujenga nyumba za muda wakati juhudi za ziada za serikali na wadau wake zikiendelea kufanyika ili kuwawezesha kujenga nyumba za kudumu katika eneo jipya walilohamishiwa na serikali ya kijiji chao
“Kitongoji kile ni eneo linalopitiwa na mkondo wa maji, na rekodi za nyuma zinaonesha wamekuwa wakisumbuliwa na mafuriko ya mara kwa mara pindi mvua za mfululizo zinaponyesha, kwahiyo serikali imefanya uamuzi wa kuwaondoa moja kwa moja, hawatakiwi kurudi tena,” alisema.
hata hivyo aliwaomba wadau wengine kuendelea kujitokeza kuungana na kampuni hiyo ya Qwihaya General Enterprises kujitolea kuwasaidia wahanga hao kurudi katika maisha yao ya kawaida kwani bado wanahitaji misaada mbali mbali mengi pamoja na ujenzi wa makazi mapya, wanahitaji pia msaada wa chakula, nguo na mahitaji mengine muhimu kuwawezesha kurudi katika maisha yao ya kawaida.
Mvua kubwa zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbali mbali ya mkoa wa Iringa na mikoa ya Njombe na Mbeya imeendelea kuleta madhara makubwa katika tarafa ya Pawaga jimbo la Isimani linaloongozwa na mbunge Wiliam Lukuvi ambae ni waziri wa Ardhi ,Nyumba na maendeleo ya makazi kutokana na eneo hilo kuwa ni uwanda wa chini zaidi usio na milima hivyo maji yamekuwa yakijaa katika tarafa hiyo mithiri ya bwawa