Taarifa zilizotufikia hivi punde zinasema kuwa, Mvua kubwa
inayoendelea kunyesha imesababisha wasafiri wanaotumia barabara kuu ya
Arusha - Dar es salaam, kupitia Kilimanjaro wamekwama kuendelea na
safari kwa zaidi ya saa mbili hadi sasa baada ya mafuriko kujaa
barabarani pamoja na vifuko na magogo.Jitihada za kuwafuta
viongozi wa Mikoa ya Arusha na Kilimanjaro inaendelea ili kujua taratibu
wanazofanya ili kuruhusu magari kuendelea na safari |
Tags:
habari