CHANGAMOTO YA FLORIDE BADO NI KUBWA ARUMERU

 Mkurugenzi wa Ngauwsa akitoa Maelezo ya Mradi wa kutibu Floradi unaondeshwa na mamlaka ya maji Safi mji mdogo wa Ngaramtoni uliofadhiliwa na shirika la Maendeleo na misaada la Uingereza Uk aid kwa vijiji vitano vya Ngaramtoni kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Auwsa Mwanasheria Edward Mroso Jana wilaani Arumeru.

Sehemu ya tanki la maji Safi yaliotibiwa kwenye mradi wa vijiji vitano kuondoa floride kwenye maji uliofadhiliwa na Ukaid uliokabidhiwa kwa Auwsa Jana wilayani Arumeru picha zote na Ahmed Mahmoud Arusha.
Aliyekuwa
Sehemu ya mitambo ya kutibu maji yenye Floride iliyokabidhiwa kwa mamlaka ya majisafi na Usafi wa mazingira Auwsa kutoka Ngauwsa 

Mkurugenzi wa Ngauwsa Claison Kimaro akiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Auwsa Edward Mroso pamoja na kaimu Mkurugenzi wa Auwsa mhandisi Justine Rujomba wakiangalia mashine za kuchuja maji yenye Floride iliyokabidhiwa kwa mamlaka hiyo Jana wilayani Arumeru picha na Ahmed Mahmoud Arusha.

Ukaguzi wa mitambo hiyo ukiendelea kabla ya makabidhiano ya mamlaka hiyo kwa Auwsa 

Sehemu ya mchoro wa mashine hizo kama unavyoonekana pichani 

Mchoro unavyoonekana pichani ni sehemu ya mashine zilizotolewa za kutibu maji yenye Floride ambayo imeelezwa maeneo mengi wilayani humo yanakabiliwa na maji yenye Floride.
Mhandisi wa mitambo hiyo akieleza utendaji wa mitambo kwa Bodi za Ngauwsa na Auwsa zilizotembelea kwenye mradi huo ikiwa ni sehemu ya makabidhiano.

Sehemu ya Jenereta la kuendesha mtambo huo pindi umeme unapokatika.

Mitambo unavyoonekana kabla ya makabidhiano hayo Jana kwenye ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Arusha Dc picha na Ahmed Mahmoud Arusha

Mhandisi wa Umeme akitoa Maelezo mbele ya Bodi za Ngauwsa na Auwsa kabla ya makabidhiano Jana kwenye ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Arusha Dc


Mgeni Rasmi Katibu Tawala wa wilaya ya Arumeru Mwalim James Nchembe akiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Auwsa Edward Mroso na Mkurugenzi wake Justine Rujomba Sanjari na Meneja wa Ruwsa mkoa wa Arusha Makaidi wakati wa  Makabidhiano kwenye ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Arusha Dc

Meza kuu wakifuatilia kabla ya makabidhiano hayo Jana kwenye ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Arusha Dc

Sehemu ya wadau wakifuatilia matukio ya makabidhiano hayo Jana kwenye ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Arusha Dc picha zote na Ahmed Mahmoud Arusha.
Na Ahmed Mahmoud na Kassim Kiko ,Arusha Dc
Mamlaka ya maji Safi ya mji mdogo wa Ngaramtoni Ngauwsa imekabidhiwa rasmi kwa Mamlaka ya majisafi na Usafi wa mazingira Auwsa ikiwa ni utekelezaji wa tangazo la gazeti la Serikali namba 661 lililotolewa na Waziri mwenye dhamana na maji tarehe 6 Mwezi wa Tisa mwaka Jana.

Akikabidhi kwa Mamlaka ya Auwsa Mkurugenzi wa Ngauwsa Claison Kimaro ameleza kuwa mamlaka hiyo imekuwa imetekeleza agizo la Serikali kuwapatia maji wananchi kwa asilimia 35 badala ya asilimia 95 kama lengo la utekelezaji wa ilani ya chama cha Mapinduzi lililoelekeza Serikali kufikia asilimia hizo katika utoaji wa huduma.

Amesema kuwa gharama kubwa ya utafutaji maji na kuyatibu sanjari na kutangaza miundombinu ya usambazaji ndio limefanya kutofikia kwenye lengo hilo na kuitaka mamlaka ya majisafi na Usafi wa mazingira Auwsa kuanzia hapo kwa kushirikiana na wadau wa maji kuweza kufikia asilimia 95 iliyopo kwenye ilani ya CCM.

Akabainisha kuwa Mamlaka hiyo imejingwe uwezo wa kutibu maji kwa kufungiwa mitambo yenye thamani ya zaidi ya bilion 8 ambayo inasamabaza maji kwenye zaidi ya kata tano zenye vijiji vitano vya awali lakini vimeongezeka hadi kufikia nane.

Kwa Upande wake Mkurugenzi wa Auwsa Mhandisi Justine Rujomba alisema kuwa Makabidhiano hayo ni utekelezaji wa agizo la waziri wa maji kupitia tangazo la gazeti la Serikali namba 661 la mwaka Jana ambalo linaitaka mamlaka hiyo kuchukuwa na kuendasha mamlaka za miji midogo ya Ngaramtoni,Usa River na Monduli.

Alisema kuwa msingi huo ndio umepelekea kuwepo kwa Makabidhiano hayo ambayo yawezesha kuanza kwa utekelezaji wa kutoa huduma za maji kwenye maeneo hayo nao kutokana na mradi unaendelea wanayo maji ya kutosha na wataendelea kuhakikisha wanafikia malengo ya ilani ya CCM kwa muda mfupi ujao.

Akawataka viongozi wa Serikali za mitaa vitongoji na madiwani kutoa habari hiyo kwa wananchi kwenye maeneo yao ili kuweza kushirikiana kufikia malengo na utoaji wa huduma Bora kwa wananchi ikiwemo usambazaji wa miundombinu yenye kukidhi matakwa na usiyopoteza maji.

Nae Katibu Tawala wa wilaya ya Arumeru Mwalimu James Nchembe kwa niaba ya mkuu wa wilaya hiyo Jerry Muro alisema kuwa ushirikiano utasaidia kuongeza ufanisi kwa kuwa anaimani kubwa na Auwsa kufikia malengo ya Serikali kuwafikishia wananchi wengi zaidi huduma za maji Safi na salama.

Alisema kuwa Auwsa ni mkubwa hivyo kama haitakuwa na ushirikiano na viongozi waliomaliza muda wao wanaweza wasifikie malengo na kuwataka kuamini kwenye ushirikiano ili kuweza kuwafikia wananchi na kuongeza wigo mpana wa utoaji huduma Bora za maji kwenye maeneo hayo.

Kwa niaba ya halmashauri ya wilaya ya Arusha Dc Diwani wa Olmotonyi alisema kuwa wanaimani kubwa na mamlaka ya majisafi na Usafi wa mazingira Auwsa kuweza kufikia malengo ya utoaji huduma zenye kukidhi kwa wananchi ambao Wana mabomba Ila hayana maji ya kutosha nanyi mmesema maji mnayo.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post