Meneja wa kampuni ya Mega Beverages Christopher Ndossi akiwa na kamanda wa Magereza Mkoa wa Arusha sanjari Mkuu wa mkoa wa Arusha Mara baada ya makabidhiano hayo ya Ndoo 50 na lita 2500 ya vikatasa mikono Leo jijini Arusha.
Na Ahmed Mahmoud Arusha
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amepokea lita 2500 za vitakasa mikono na ndoo 50 za kuoshea mikono Sanjari na hundi za fedha ikiwa ni sehemu ya mapambano dhidi ya ugonjwa wa Covid 19.
Kwa muktadha huo ameendelea kuwataka wananchi kuendelea kuchukuwa hatua za kudhibiti Ugonjwa wa Covid 19 kwa kufuta maelekezo na kuacha misongamano isiyo ya lazima.
Akiongea wakati wa Makabidhiano hayo kutoka kampuni za Mega Beverages Hanspaul na Simba Truck Gambo alisema kuwa wananchi wanatakiwa kuendelea kuchukuwa hatua zaidi za kujikinga na maambukizi ya ugonjwa huo zinazoelekezwa na Serikali
Alisema kuwa kila mmoja wetu tuache kukusanyika kwenye maeneo yenye misongamano isiyo ya lazima na kuwataka wenye mabasi daladala kuacha kujaza na kuendelea kuchukuwa hatua kwa kuweka maji tiririka vituoni.
"Kama Serikali tunawashukuru Sana wadau hawa ambao wameonyesha kushirikiana nasi katika kukabiliana na janga hili la Ugonjwa wa Covid 19 nasi tutaendelea kuchukua hatua zaidi za kukabiliana na ugonjwa huu"
Alisema kuwa wananchi tusijiamini Sana kwa kuwa Ugonjwa huo unaua kwa kuepuka misongamano isiyo ya lazima na kuzingatia maelekezo yanayotolewa na Serikali huku akibainisha kuwa wanahitaji kiasi cha milioni 196 za ukarabati wa eneo la wagonjwa kama walivyoelekezwa na Waziri wa Afya na shirika la Afya Ila la awali limekamilika.
Awali Katibu Tawala wa mkoa wa Arusha Richard Kwitega alisema kuwa tangia tukio la kwanza kutangazwa wamekuwa wakishirikiana na wadau jinsi ya kupata vifaa sanjari na utoaji wa elimu ikiwemo ushiriki wa juu ya mapambano ya Covid 19.
Alisema kuwa kumekuwa na mahitaji mengi ya vifaa ndani ya jamii yetu na kama Serikali imeendelea kushirikiana na wadau mbali mbali kuona jinsi ya kusaidiana kupata vifaa kuisaidia jamii.
Kwa Upande wao Meneja wa Mega Beverages Christopher Ndossi na Mkurugenzi wa Hanspoul na Mkurugenzi wa Simba Truck wamesema kuwa wataendelea kushirikiana na Serikali katika kuhakikisha wanaendeleza kupambana Ugonjwa huo na huo ni mwanzo wa msaada huo.
|