KAMPUNI YA NGUZO ZA UMEME YA QWIHAYA YATOA VIFAA KINGA YA CORONA KWA POLISI MUFINDI

Mkuu wa polisi wilaya ya Mufindi Abichi Masanga akiwakabidhi askari wake vifaa kinga vya Corona vilivyotolewa na kampuni ya Qwihaya 

Meneja wa kampuni ya Qwihaya General Enterprises Ltd Ntibwa Mjema akimkabidhi mkuu wa polisi wilaya ya Mufindi Abichi Masanga msaada wa vifaa vya kujikinga na Corona askari .
................
KAMPUNI  ya kizalendo ya Qwihaya  General Enterprises Ltd inayozalisha nguzo za umeme imelikumbuka jeshi la Polisi mjini Mafinga, wilayani Mufindi kwa kutoka vifaa vya kujikinga na maambukizi ya virusi vya corona .

Msaada huo ni mwendelezo wa ziara ya Qwihaya katika kukabidhi vifaa hivyo maeneo mbalimbali na tayari zaidi ya Sh65 zimetumika kwa kazi hiyo tangu janga hilo lianze.

Akikabidhi msaada huo, Meneja wa Qwihaya, Ntibwa Mjema amesema kampuni hiyo imeamua kushiriki kwa vitendo vita dhidi ya corona ikiunga mkono jitihada za Serikali katika kupambana.

Tumetoa vitakasa mikono, barakoa na sabuni ili wenzetu polisi wanapotekeleza majukumu yao wawe kwenye mazingira salama," amesema Mjema.

Kwa upande wake, Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Mufindi, Abichi Masanga aliishukuru kampuni hiyo na kuziomba kampuni nyingizi ziige mfano huo.

"Tunashukuru kwa huu msaada na bado tunahitaji msaada mwingine, hapa wanakuja raia wengi na watuhumiwa wakiwa hapa wanahitaji barakoa na sanitaiza kwa hiyo, mahitaji makubwa" amesema Kamanda Masanga.

Kwa sasa kampuni ya Qwihaya inamilikiwa na Mzalendo, ndugu Leonard Mahenda ina viwanda vya kuzalisha nguzo za umeme katika mikoa ya Iringa na Kigoma huku mkakati ukiwa kumaliza uhaba wa bidhaa hiyo ambayo awali ilikuwa ikiingizwa kutoka nje ya nchi unamalizika.

 Kampuni hiyo umesema kauli mbiu yake kubwa ni Qwihaya umeme unawaka vijijini kama mijini
Mwisho.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post