Baadhi ya mashine zilizokuwa zikitumika kusaga kahawa zikiwa zimeteketea kabisa kwa moto |
Wananchi wakishuhudia sehemu ya kiwanda hicho kikiwa kimeteketea kwa Moto |
Na Clavery Christian Karagwe
Kagera.
Zaidi ya mashine 22 zenye
thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 1.6 za kiwanda cha kukoboa kahawa cha
Amuri Amir kilichopo katika kata ya Kayanga wilayani Karagwe mkoani kagera pamoja
zimeteketea kwa moto kutokana na ni hitilafu ya umeme.
Akizungumuza katika eneo
la tukio mmiliki wa kiwanda hicho Kharim Amuri amesema kuwa tukio la kuungua kwa
kiwanda chake limetokea mei 7 mwaka huu majira ya saa kumi na moja alfajiri
wakati mvua kubwa iliyokuwa imeambatana na radi kunyesha huku kiwanda
hicho kikiwa kimefungwa.
Amuri amesema kuwa baada
ya kufika eneo la tukio kwa kushirikiana na majirani walianza kuzima moto huo
kabla ya kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya Karagwe kufika eneo la tukio ikiwemo
jeshi la zimamoto mkoa Kagera.
Naye Thomas
Majuto ambaye ni mkaguzi wa jeshi la zimamoto na afisa oparesheni zimamoto
mkoa Kagera amesema kuwa uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa chanzo cha
moto huo ni hitilafu ya umeme.
Hata hivyo mkuu wa mkoa wa
Kagera Brigedia Generali Marco Elisha Gaguti
baada ya kufika katika eneo la tukio ametoa pole kwa uongozi wa kiwanda hicho na
kusema kuwa uongozi wa mkoa huo utatoa ushirikiano katika
kipindi hiki kigumu hadi kiwanda hicho kitakaporejea upya na kuanza kufanya kazi.