Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya akiwa na viongozi wa CCM wilaya ya Hai |
KADA wa, Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Hai, Dk. Saashisha Mafue, amesshinda kura za maoni za wanachama wa chama hicho baada ya kuwabwaga wenzake 41waliowania fursa ya kupeperusha bendera ya chama hicho katika kinyang'anyiro cha ubunge kwenye uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu.
Akitangaza matokeo ya kura hizo za maoni, Msimamizi wa Uchaguzi, Shukuru Kataba amemtaja Mafue kuwa anefanikiwa kupata kura 124 kati ya 449 akifuatiwa na mbunge wa zamani wa jimbo hilo,Futa Kimbita ambaye alipata kura 85 katika mkutano mkuu uliofanyika mjini Bomang'ombe mapema leo.
Mwanachama Abubakar Msangi alifuatia kwa kupata kura 48 huku mwakilishi wa Kampuni ya magazeti ya serikali (TSN) tawi la Arusha, Edna akiwa wa nne baada ya kujizolea kura 47 katika kura hizo zilizokuwa na ushindani mkubwa.
Katiba alimtangaza Everlight Swai kuwa ameshika nafasi ya tano baada ya kupata kura 20 katika kura hizo.
Mwenyekiti wa zamani wa UVCCM wilaya ya Arusha, Martin Munisi ambaye pia ni diwani wa Machame Magharibi aliambulia kura 15 katika kinyang'anyiro hicho.
Iwapo atapitishwa na vyombovya uteuzi vya chama chake, Mafue anatarajiwa kupambana na mbunge wa sasa wa jimbo la Hai, Freeman Mbowe ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).