Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi ametaja siri 10 zilizopelekea Tanzania kuingia katika uchumi wa kati miaka mitano kabla ya lengo.
Amesema Tanzania imekua miongoni mwa nchi 50 Duniani, nchi ya 24 kwa Afrika na ya pili kwa Afrika Mashariki kuingia katika uchumi wa kati, Uchumi wa kipato cha kati umehusishwa na nchi ambayo umasikini unapungua, uchumi imara unajengwa, uzalishaji viwandani unaimarika na wananchi wanapata maendeleo.
“Hii ni kali zaidi, tumewekeza katika maendeleo ya watu moja kwa moja, tukapimwa na benki ya Dunia tukaonekana tupo kwenye wastani wa kipato cha kati, Misingi kumi iliyotusaidia kuingia katika kipato cha kati ni amani na utulivu, mipango thabiti ya maendeleo, utekelezaji usioyumba, kufanya maamuzi magumu,azma ya kujitegemea, nidhamu katika matumizi”