RUSHWA YAELEZWA KUTUMIKA KUPITISHA WAGOMBEA KURA ZA MAONI ARUSHA

Mmoja waliokuwa wakiwania nafasi ya kura za maoni ndani ya CCM Mrisho Gambo wa pili kulia akihesabu kura za wajumbe kabla ya kutangazwa mshindi katika kinyang'anyiro hicho kwa kura 333 kati ya kura 481 za wajumbe waliopiga kura.
Na Mwandishi Wetu, Arusha.

Malalamiko ya kukithiri kwa rushwa na upendeleo kwa baadhi ya wagombea wakati wa kujinadi katika kura za  maoni za Jimbo la Arusha Mjini, yametawala mioyo na midomo ya wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM wa wilaya hiyo.

Wengi wa wajumbe 481 waliohudhuria mkutano huo wanaeleza wazi kusikitishwa na hatua ya Mwenyekiti wa, mkutano huo Mary Kisaka kukataa baadhi ya wagombea kuulizwa maswali wakati wakiomba kura.

Wanamlenga hasa mgombea Mrisho Gambo ambaye baada ya kujieleza, mbele ya wajumbe, Mwenyekiti huyo wa kikao alikataa asiulizwe maswali, kama ilivyokuwa kwa wengine, hata iliyozuka manung'uniko ukumbini.

" Si haki wala sawa hata kidogo..hapa kuna mchezo mchafu unaendelea kati ya Mama Kisaka (mwenyekiti wa mkutano) na Mrisho Gambo na lazima suala hili lifike kwa Polepole (Katibu wa Siasa na Itikadi Taifa).Hatukubali demokrasia yetu ibakwe mchana, hadharani," amesisitiza mjumbe kutoka Kata ya Olerien na kuongeza:
"Rushwa ilitolewa bila kificho na, wafuasi wa mgombea mmoja(jina linahifadhiwa)  walikuwa wakigawa kuanzia sh.150,000 hadi 200,000) kwa kila mjumbe kama kishawishi cha kuomba kura.

Akitangaza matokeo ya kura hizo za maoni, Msimamizi wa Uchaguzi huo, Molloimet ole Moko amemtangaza Mrisho Gambo kuibuka kidedea akipata kura 333 akifuatiwa na Philemon Mollel (Monaban) aliyepata kura 68 akifuatiwa na Wakili maarufu Albert Msando alyeijipatia kura 19
Meya wa zamani wa Jiji la Arusha, Calist Lazaro aliambulia kura 2 huku Meya mwingine wa zamani wa jiji hilo, Gaudence Lyimo akitia kibindoni kura 13.

Katika jimbo la Arumeru Magharibi, Noel Severe ameinuka kidedea kwa kura 113  dhidi wagombea wenzie 32 katika chaguzi za kura za maoni katika jimbo hiloi ili kugombea nafasi ya ubunge kupitia Chama Cha mapinduzi(CCM) katika Uchaguzi mkuu unatarajiwa kufanyika Octoba 25,Mwaka huu.

Mkutano huo wa uchaguzi ulioudhuriwa na wajumbe 611 huku Severe akipata kura nyingi zaidi ya wenzie kutoka kata 27 za  Ortument, Lengijave, Sambasha, Musa,  mateves, Oldonyosambu, Kisongo, Mwandeti, Kiutu, Kimnyaki, Bangata, Olkokola, Moivo, Olorieni, Kiranyi, Ilkiding'a, olturoto, laroi, Lemanyata,Olmotonyi,Sokoni ii, Orjoro, ilboru, Mlangarini,Tarakwa na Bwawani.

Akitangaza matokeo hayo katika mkutano huo   wa jimbo, msimamizi wa Uchaguzi,Naftal Robert alisema jumla ya kura zilizopigwa ni 605 na zilizoharibika ni 6.

Severe amefuatiwa na Joseph Lukumay(66), David Sigara (59),Furaha Lekoko( 54 ),Noah Saputu (44) na Amina Mollel( 41).

Mbunge wa zamani wa jimbo hilo Goodluck Ole Medeye aliambulia kura 14.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post