WANANCHI KATA YA KALOLENI ENEO LA TANKI LA MAJI WAZIOMBA MAMLAKA KUINGILIA KATI UWEPO WA DANGURO ENEO HILO


Sehemu ya nyuma ya nyumba ambayo Inadaiwa na wananchi hao kuwepo kwa danguro la vijana wanaotumia madawa ya kulevya na kufanya vitendo vya Ngono na kusababisha uvunjifu wa amani na utulivu katika eneo la mita miambili Tanki la maji kata ya Kaloleni jijini Arusha kama lilivyokutwa na kamera ya matukio jijini Arusha 

Muonekano wa Nyumba hiyo ambayo wanaishi vijana kwa madai ni hosteli na kuitumia kama Danguro kama ilivyokutwa na kamera ya matukio jijini Arusha mapema leo 
Na Ahmed Mahmoud Arusha
Wananchi Kata ya Kaloleni jijini Arusha wamelalamikia kuwepo kwa danguro lililopo eneo la tanki la maji mita Mia mbili ambalo limekuwa kero kubwa kwao hali inayoplekea kuhatarisha amani na utulivu kwao. Aidha uwepo wa Danguro hilo umekuwa adhaa kubwa kutokana na kelele za watumiaji wa dawa za kulevya wanaotumia mwanya huo kuwavutia wanawake ndani kwa nguvu na kufanya nao vitendo vya ngono. Akizungumza na Waandishi wa habari mmoja ya wananchi hao Mussa Said alisema kuwa .makazi hayo ya Danguro hilo yamekuwa kero kubwa kwao hususani wanafunzi ambapo amezitaka mamlaka kuchukuwa hatua za haraka kuondoa hali hiyo. Alisema makazi yao ni eneo la mita 200 ambalo kila wakati wanapambana na Vijana wanaoishi katika daquro hilo kupiga kelele kuvuta bangi na kuvutia Wanawake Ndani Kwa nguvu na kufanya nao ngono Wakitoa Malalamiko yao wananchi hao wamesema kwamba Kwa muda takribani Miaka miwili kuna Daquro amabalo Vijana wakiume hujikusanya na kukaa pamoja Kwa Madai kuwa ni hostel ya kujisomea kama wanafunzi kumbe wamegeuza eneo hill kuwa sehemu ya kufanyia ukahaba kuvuta bangi na kupiga muziki Kwa Sauti ya Juu Hata hivyo Taarifa zilizofanyiwa Kazi Ndani ya eneo hill linalomilikiwa na mwanamke moja ambaye makazi yake ni jijini Dar es saalam aliye tambulika Kwa jina la halima Mamiro zinasema kwamba kuwepo Kwa daquro hilo imekua ni changamoto kwako Moja wa mwananchi aliyejitambulisha Kwa jina la Linda Mathayo amesema kwamba kuwepo Kwa hostel hivyo bubu katika makazi ya wananchi bila kufuata taratibu za usajili ni kukera wakazi na jambo linalohatarisha maisha Kwa watoto wao hususani wanafunzi. “Sisi kama wakazi wa eneo hili Kwa kweli tunapata shida kwani Vijana wanaishi katika eneo hili tumetafuta uwongozi wa serikali za Mtaa kutusaidia lakini akuna Msaada wowote tulio upata zaidi ya siku moja tu bwana Afya kuja kutembelea daquro na kuondoka bila kutoa majibu yoyote kwetu tunaomba kupitia wiraza ya nyumba na makazi kusikia kilio chetu” Linda ameeleza kwamba viongozi wa serikali za Mtaa wameshindwa kutatua kero hivyo kwani wamekua wakihongwa pesa na miliki wa nyumba hi\yo na kuzima changamoto hizo zinazo wakabili wananchi hao.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post