TUNDU LISSU AREJEA NCHINI, WANACHADEMA WAMPOKEA KISHUJAA

Makamu Mwenyekiti Chadema Tundu Lissu (katikati) akiwasili uwanja Ndege JK Nyerere. Kushoto Freeman Mbowe na John Mnyika (kulia).

Makamu Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Upinzani nchini Tanzania Chadema- Bara  Tundu Antiphas Lissu amewasili nchini leo Jumatatu tarehe 27 Julai 2020 huku kila mmoja alitaka kumsogelea amguse Lissu.

Lissu amewasili nchini Tanzania akitokea Ubelgiji kwa ndege ya Shairika la Ethiopia na kupokelewa na viongozi wa Chadema, ndugu, jamaa na marafiki katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam.

Baada ya kuwasilia, umati ya watu waliojitokeza kumpokea mwanasiasa huyo, umeanza msafara kutoka uwanjani hapo kwenda Ofisi za Makamu Makuu ya Chadema, mtaa wa Ufipa, Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Mara baada ya kutoka ndani akiwa ameongozana na viongozi wa Chadema akiwemo Freeman Mbowe, mwenyekiti wa chama hicho na Katibu Mkuu wake, John Mnyika, shangwe zilitawala uwanjani hapo.

Sauti za nyimbo zilisikika zikiimba ‘Rais, Rais, Rais, Rais’ hali iliyowafanya walinzi kutumia nguvu kuwaweka kando.

Lissu amerejea nchini mwake ikiwa imepita miaka takribani mitatu tangu alipokuwa nje ya nchi kwa matibabu baada ya kushambuliwa na watu wasiojulikana kwa risasi zaidi ya 30.

Tukio hilo lilitokea mchana wa tarehe 7 Septemba 2017 katika makazi yake Area D jijini Dodoma na kupelekwa Hospitali ya Rufaa Dodoma kwa matibabu.

Usiku huohuo alisafirishwa akiwa hajitambui kwenda Hospitali ya Nairobi nchini Kenya kwa matibabu zaidi hadi tarehe 6 Januari 2018 alipohamishwa nchini Ubelgiji kwa matibabu zaidi.




This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post