JAJI MRUMA AMESEMA WANANCHI HAWAJUA HAKI NI KITU GANI

 


IMG_9648
JAJI Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Tanga,Amir Mruma akizungumza wkati wa ufunguzi wa maadhimisho hayo


IMG_9595
Naibu katib u Mkuu Wizara ya Sheria na Katiba Amon Mpanju akizungumza wakati wa ufunguzi wa maadhimisho hayo


IMG_9637
Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shgella akizungumza wakati wa ufunguzi wa maadhimisho hayo

_MG_9614AMINA SAIDI,TANGA

JAJI Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Tanga,Amir Mruma amesema wananchi hawajui haki ni kitu gani  anapaswa kuambiwa na polisi kabla ya kukamatwa na kwamba nguvu ya ziada itatakiwa kutumika ikiwa mkamatwaji anakataa kwenda kuripoti kituo cha polisi.

Mruma ametoa kauli hiyo akimwakilisha Jaji kiongozi Dk Elieza Fleshi katika maadhimisho ya wiki ya msaada wa kisheria ambayo kitaifa yanafanyika jijini Tanga.

Jaji Mruma alisema kuwa wananchi pia hawajui haki ya kujua ni muda gani anapaswa kukaa kituo cha polisi kabla ya kufikishwa mahakamani kwa ajili ya kusikiliza shauri lake.

“Baadhi ya wananchi wanadhani kuwa kukamatwa na polisi ni shariti ,upigwe makofi na mateke na  kurushwa kichura,jambo ambalo halipo kisheria,na katika wiki hii wananchi wataelimishwa juu ya haki yao ya kisheria wanapokutana na mazingira ya aina hiyo"alisema Jaji Mruma.

Kwa upande wake Naibu katib u Mkuu Wizara ya Sheria na Katiba Amon Mpanju aliwataka watanzania kuwa na utaratibu wa kuandika wosia wakati wakiwa hai ili kuepusha migogoro ya kifamilia ambayo imekuwa ikiibuka mara baada ya mzazi kufariki dunia.

“Migogoro mingi imekuwa ikitokea mara baada ya mzazi kufariki dunia na hasa hasa ni pale ambapo mzazi anakuwa hajaacha wosia wa aina yoyote,jambo hilo ni muhimu sana kwa kuwa likifanyika hata baada ya mzazi kutopeza maisha hakutakuwa na shida"alisema Amoni.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shgella aliwataka wananchi kuyatumia maadhimisho hayo kwenye kutatua migogoro ya ardhi katika maeneo yao ikiwa ni pamoja na  kuwasikiliza wataalamu wa masuala ya kisheria  na kupata shauri ambao utamaliza migogoro yao.

Katika wiki nzima ya maadhimisho haya ambayo inatarajiwa kufikia kilele  Novemba 17 mwaka huu wataalamu wa kisheria watakutana na makundi mbalimbali ya kijamii katika mkoa wa Tanga na kutoa uelewa wa kisheria.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post