NAIBU GAVANA (BOT) AIPONGEZA TFA KWA KUSAMBAZA PEMBEJEO BOR

 Wananchi wakisikiliza hotuba ya Naibu Gavana


Na. Vero Ignatus ,Arusha.

Naibu Gavana wa Benki kuu Tanzania (BOT) Dr.Yamungu Kayandabila amekipongeza Chama cha Wakulima Tanganyika (TFA) kwa kusambaza pembejeo bora kwa Wakulima hivyo kuongeza uzalishaji na kusaidia upatikanaji wa malighafi katika viwanda .

Akifungua Mkutano Mkuu wa Chama cha Wakulima Tanganyika (TFA),Naibu Gavana amekitaka chama hicho kuendelea kushirikiana na taasisi za fedha katika kukuza kilimo ili kuinua pato la mkulima na taifa kwa ujumla.

Dr.Yamungu amesema kuwa katika safari ya uchumi wa viwanda wakulima ni wadau muhimu ambao wanapaswa kuhakikisha kuwa wanazalisha malighafi kwa wingi.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi  wa TFA, Peter Sirikwa  amesema kuwa walainza kusambaza pembejeo kwa wanachama wao na wanampango wa kuwafikia wanachama 5000 na wakulima walioko nje ya chama hicho.

“Tunaomba serikali itasaidia kuweka mazingira mazuri ya uagizaji wa pembejeo kutoka nje ili wakulima wetu wapate pembejeo bora na kwa gharama nafuu” Alisema Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Peter Sirikwa.

Mkurugenzi Mtendaji wa TFA, Jastin Shirima amesema kuwa mpango wao ni kuwafikia wakulima wengi na kusambaza pembejeo ambapo kwa sasa wana vituo 17 nchini vya kusambaza pembejeo.

Kwa upande Wake Mkulima aliyehudhuria Mkutano huo  Anselim Antony ameipongeza TFA kwa mpango huo kwani utawawezesha wakulima kuondokana na pembejeo feki.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post