RC Arusha ataka kampuni za Utalii na mahoteli kupunguza bei kwa Watalii wa ndani

 Mussa Juma,

Arusha.Mkuu wa mkoa wa Arusha,Idd Kimanta amewataka wamikili wa kampuni za Utalii na mahoteli mkoani Àrusha kupunguza bei ili kuvutia Watalii wa ndani kutembelea hifadhi za Taifa.


Akizungumza na Wafanyakazi 80 wa benki ya CRDB ambao wametoka jijini Dar es salaam kuelekea mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro kutalii, leo November 13 Kimanta amesema gharama kubwa kutembelea hifadhi kunapunguza  Watalii wa ndani.


"Wakati huu Taifa linakabiliwa na upungufu wa Watalii kutoka nje ni vizuri wenye kampuni za Utalii mtusaidie kushusha gharama za magari,chakula na kulala hifadhi Watalii wa ndani"amesema


Awali Mkurugenzi wa masoko wa Bodi ya Utalii nchini(TTB)Mindi Kasiga amesema Bodi hiyo kwa kushirikiana na CRDB wameweza kuanzisha kampeni za kuhamasisha Utalii wa ndani.


"Kampeni hii ya tembelea Mbuga zetu pia inahusisha shirika la ndege nchini(ACTL)kampuni ya Zara Tours na Mamlaka ya viwanja vya ndege"amesema


Afisa Masoko Mkuu wa Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), Michael Makombe amesema Wafanyakazi hao wa CRDB hawatajutia muda na gharama za kutembelea Ngorongoro kwani kuna vivutio vingi


"Wakiwa Ngorongoro watashuhudia wanyama wakubwa Tembo,Simba,Nyati ,Faru  wakiwa katika eneo la Creta"amesema


Amesema pia watajionea maajabu ya Ngorongoro ikiwepo mchanga unaotembelea,makumbusho ya Olduvai na kreta ya Embakai.


Katibu Mkuu wa Chama cha Mawakala wa Utalii(TATO) Sirili Ako amepongeza CRDB kwa kuanzisha utaratibu kupeleka Wafanyakazi hifadhini na ametaka taasisi nyingine kuiga ili Wafanyakazi waone utajiri wa Maliasili za Taifa na kuokoa sekta ya utalii.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post