Urais wa UTPC, mitano tena kwa Deo Nsokolo

Wajumbe wa Mkutano Mkuu wakifuatilia mkutano
Rais wa UTPC Deo Nsokolo ambaye amechaguliwa kwa miaka mingine mitano kuwa Rais wa Muunganiko wa umoja huo
Mwenyekiti wa Arusha Press Club APC, Claud Gwandu akipiga kura katika uchaguzi huo, Gwandu pia alichaguliwa kuwa mjumbe wa bodi ya UTPC

 Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoa wa Kigoma, Deogratius Nsokolo ameshinda tena nafasi ya Urais wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) katika uchaguzi uliofanyika leo Mkoani Morogoro wakati wa Mkutano mkuu wa UTPC. 

Katika uchaguzi huo jumla ya wajumbe 83 wamepiga kura ambapo Bw. Nsokolo amepata kura 72 huku Mpinzani wake Edwin Soko ambaye ni Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa habari mkoa wa Mwanza akiambulia kura 11.

Kwa matokeo haya Deogratius Nsokolo atatumikia nafasiya Urais UTPC kwa miakka mingine mitano kuanzia 2020-2025 baada ya kutumikia miaka mingine mitano 2015-2020.

Matokeo kwa ujumla haya hapa:


Wagombea wanawake

Walioshinda nafasi ya ujumbe wa bodi ya wakurugenzi UTPC ni

1. Hadija Omar 48

2. Lilian Lucas 51

3. Salma Abdul 62

4. Paulina David 63

Jumla ya kura zilizopigwa ni 83

Wagombea nafasi za ujumbe Bodi ya Wakurugenzi UTPCW anaume  walioshinda ni

1. Mussa Yusuf 51

2. Cloud Gwandu 61

3. Frank Leonard 64

4. Abdallah Mfaume 69

Kura zilizopigwa ni 83


Kundi la wataalam alikuwa mgombea mmoja

Eliazer Mafuru kapata kura zote 83 za ndiyo


Kura za Makamu wa Rais UTPC

Wagombea ni

1. Lulu George 18

2. Pendo Mwakyembe 65

Kura halali ni 83


Kura za Rais wa UTPC 

1. Deo Nsokolo 72

2. Edwin Soko 11

Kura halali 83

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post