Wakenya, Watanzania wamshambulia Odinga, ushauri wake kwa JPM kuhusu CORONA

 

Raila Odinga, Waziri Mkuu Mstaafu wa Kenya 

Na Mwandishi Wetu, Arusha

BAADA ya aliyekuwa Waziri Mkuu wa Kenya Raila Odinga kusema kuwa Rais wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli anashauriwa vibaya kuhusu mlipuko wa ugonjwa wa Corona, wasomaji mbalimbali wamepingana vikali na kauli hiyo na kusema kuwa Rais Magufuli yuko sahihi na aachwe na msimamo wake.

Wakichangia katika ukurasa wa kituo cha redio cha BBC ambacho ndicho kilichorusha taarifa hiyo baada ya kufanya mahojiano na kiongozi huyo wa Kenya, mmoja wa wakenya amesema Raila hana jambo ambalo anaweza kumshauri Rais Magufuli katika CORONA kwa kuwa Tanzania ndio nchi pekee inayoonyesha njia ukanda wa Afrika.

Mchangiaji mwingine anayejiita, JPM forever ameandika kuwa, “BBC mtuache sisi ndio wapiga kura wake, nyie inawauma nini fanyeni yanayowahusu ya JPM mtuachie sisi na mwaka huu tunamchagua tena, ili iwaume zaidi fungeni midomo sisi watanzania tunamkubali Rais wetu na tupo nae katika kipindi ichi sio yeye aliyeleta corona mngekuwa wa maana mngejadili aliyeileta hii corona duniani “.

Aliongeza, “Kama habari hamna njooni niwape habari za yesu anavyoipigania Tanzania na alivyokaribu na Rais wetu, hii nchi inaongozwa na Mungu na Rais wetu anaongozwa na Mungu na pia wananchi wake tunaongozwa na Mungu sisi atumtegemei binaadam katika kuendesha taifa letu bali tunamtegemea Mungu kila mtu kwa imani yake, kwa hiyo kama mnataka kutuchonganisha watanzania sio wajinga na ndio maana hizo comment zote zinawakandamiza nyie BBC na kwa waandishi wenu wenye chuki na taifa letu,”.

Waliomba kiongozi huyo wa Kenya kujadili masuala yanayoendelea nchini kwake na kuiacha Tanzania ikiendelea kupambana na hali ya ugonjwa huo ambao kihalisia haupo nchini baada ya Rais kuamua kufanya maamuzi magumu.

Tangu kulipoibuka kwa ugonjwa wa CORONA mapema machi mwaka huu, tayari maelfu ya watu duniani wamefariki duniani huku ugonjwa ukiendelea kusambaa maeneo mengi Zaidi duniani. 

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post