Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji, Mhe. Dkt.Christina Ishengoma akizungumza na wananchi wa kijiji cha Msisiri kilichopo Kata ya Chipogolo wilayani Mpwapwa wakati kamati hiyo ilipotembelea kijijini hicho pamoja na kusikiliza kero za wavuvi na wananchi kuhusu maendeleo ya Bwawa la Mtera ziara iliyofanyika leo Juni 19,2021.
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Rashid Tamatamah akijibu maswali ya wananchi wa kijiji cha Msisiri kilichopo Kata ya Chipogolo wilayani Mpwapwa wakati Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji ilipotembelea kijijini hicho pamoja na kusikiliza kero za wavuvi pamoja na wananchi kuhusu maendeleo ya Bwawa la Mtera ziara hiyo imefanyika leo Juni 19,2021.
Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Msisiri wakifatilia hotuba mbalimbali wakati wa Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji,ilipofanya ziara ya akizungumza na wananchi wa kijiji cha Msisiri kilichopo Kata ya Chipogolo wilayani Mpwapwa pamoja na kusikiliza kero za wavuvi na wananchi kuhusu maendeleo ya Bwawa la Mtera ziara iliyofanyika leo Juni 19,2021.
Mfanyabiashara wa Kijiji cha Msisiri Bi.Nelly Athuman akitoa maoni yake kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji ilipotembelea kijiji hicho kilichopo wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma leo Juni 19,2021.
Mtendaji wa Kijiji cha Msisiri Bw.Allan Kayanda,akielezea changamoto zilizopo katika kijiji hicho kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji ilipotembelea kijiji hicho kilichopo wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma leo Juni 19,2021.
Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji ambaye pia ni Mbunge wa Mvumi, Livingstone Lusinde (CCM) akitoa mapendekezo yake kwa wananchi wa kijiji cha Msisiri kilichopo wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma mara baada hiyo kutembelea kijiji hicho kuhusu Maendeleo ya Bwawa la Mtera leo Juni 19,2021.
Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum (Chadema) Kunti Majala,akitoa maoni yake kwa kamati hiyo amabyo ilifanya ziara ya kutembelea kijiji hicho kuhusu Maendeleo ya Bwawa la Mtera leo Juni 19,2021.
Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Msisiri kilichopo wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma wakati wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji ilipotembelea kijijini hicho pamoja na kusikiliza kero za wavuvi pamoja na wananchi kuhusu maendeleo ya Bwawa la Mtera ziara hiyo imefanyika leo Juni 19,2021.
Muonekano wa Bwawa la Mtera.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji, Mhe. Dkt.Christina Ishengoma akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mnadani Kata ya Izazi wilayani Iringa Mkoani Iringa baada ya kamati hiyo kufanya ziara ya kuzungumza na kusikiliza kero za wananchi hao kuhusu maendeleo ya Bwawa la Mtera ziara iliyofanyika leo Juni 19,2021.
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Rashid Tamatamah,akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mnadani Kata ya Izazi wilayani Iringa Mkoani Iringa baada ya kamati ya kudumu ya bunge ya Kilimo,Mifugo na Maji kufanya ziara ya kuzungumza na kusikiliza kero za wananchi kuhusu maendeleo ya Bwawa la Mtera ziara iliyofanyika leo Juni 19,2021.
Mvuvi wa Samaki Bw.Amir Kiselo,akitoa maoni yake kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji ilipotembelea kijijini cha Mnadani Kata ya Izazi wilayani Iringa Mkoani Iringa kuhusu Maendeleo ya Bwawa la Mtera ziara iliyofanyika leo Juni 19,2021.
Afisa Uvuvi Kata ya Izazi Onesmo Peter,akielezea changamoto wanazozipata wavuvi katika Bwawa la Mtera kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji ilipotembelea kijijini cha Mnadani Kata ya Izazi wilayani Iringa Mkoani Iringa kuhusu Maendeleo ya Bwawa la Mtera ziara iliyofanyika leo Juni 19,2021.
Mama Ntilie Bi.Mary Mgata ,akitoa shukrani kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji mara baada ya kuwatembelea na kuwasikiliza kero zao wananchi wa kijiji cha Mnadani Kata ya Izazi wilayani Iringa Mkoani Iringa kuhusu Maendeleo ya Bwawa la Mtera ziara iliyofanyika leo Juni 19,2021
Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Mnadani Kata ya Izazi wilayani Iringa Mkoani Iringa wakiisikiliza Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji,ilipofanya ziara ya akizungumza na wananchi wa kijiji hicho kuhusu maendeleo ya Bwawa la Mtera ziara iliyofanyika leo Juni 19,2021.
Na.Alex Sonna,Iringa
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji imeridhishwa na elimu iliyotolewa kuhusu uvuvi haramu kwa wavuvi wa Bwawa la Mtera.
Hayo yamesemwa leo Juni 19,2021 na Mwenyekiti wa kamati hiyo, Dkt. Christine Ishengoma baada ya kamati hiyo kufanya ziara katika kijiji cha Msisiri wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma na kijiji cha Mnadani wilaya ya Iringa ambapo wamezungumza na wavuvi na wananchi wa maeneo hayo.
Dkt. Ishengoma amesema katika vijiji vyote walivyopita wamekuta wavuvi na wananchi kwa ujumla wanayo elimu kuhusu uvuvi haramu na wanashiriki katika kudhibiti kwa kukamata nyavu haramu na kuziteketeza.
''Kwa kweli sisi kamati baada ya kuzungumza na wananchi pamoja na wavuvi wa maeneo yote hayo mawili tuliyotembelea tumeridhishwa na elimu iliyotolewa kuhusu uvuvi haramu kwa wavuvi wa Bwawa la Mtera''amesema Dkt.Ishengoma
Hata hivyo Dkt.Ishengoma amewataka wavuvi kuendelea kudhibiti uvuvi haramu katika Bwawa hilo ambalo kwa sasa samaki wamepungua katika baadhi ya maeneo kutokana na Uvuvi haramu.
Dkt. Ishengoma amewaahidi wananchi wa kijiji cha Mnadani kuwa atalifikisha tatizo la wingi wa viboko katika Bwawa hilo kwa Waziri wa Maliasili na Utalii ili aweze kulishighulikia.
Kwa upande wake Katibu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Sekta ya Uvuvi, Dkt. Rashid Tamatamah amesema kuwa wizara imekuwa ikitoa elimu kuhusu uvuvi haramu na madhara yake kwa wavuvi na wananchi wanaolizunguka Bwawa la Mtera ambapo kwa sasa wananchi hao wamekuwa wakishirikiana na serikali kudhibiti na kuteketeza nyavu zisizofaa zilizokamtwa.
Dkt. Tamatamah amewaahidi wavuvi wa kijiji cha Msisiri kuwaletea injini moja ya boti mwezi Julai, 2021 ambayo pamoja na shughuli za uvuvi itawasaidia katika kufanya doria za kudhibiti uvuvi haramu.
Pia amesema kuwa atawatuma wataalam wa utafiti kutoka TAFIRI kuja kuangalia kutafiti Kama upo uwezekano wa kuweka mbegu ya samaki ili kusaidia kuongeza wingi wa samaki katika Bwawa hilo.
Dkt. Tamatamah amewasisitiza wavuvi kujiunga kwenye vyama vya ushirika ili waweze kukopesheka na kuweza kupata zana sahihi za uvuvi ambazo mara nyingi hutolewa na wizara.
Naye Mkazi wa kijiji cha Mnadani kata ya Izazi wilayani Iringa, Bw. Amiri Kiselo ameieleza kamati hiyo kuwa viboko katika bwawa hilo wameongezeka na wamekuwa wakijeruhi na hata kuwauwa wavuvi na kuwafanya kushindwa kwenda kuvua Samaki.
''Tatizo hili limefanya samaki kuwa wachache katika masoko na kuwafanya wavuvi kutafuta shughuli nyingine za kuwaingizia kipato na hivyo ameiomba kamati kuwasaidia kulitatua tatizo hilo.
Wananchi katika vijiji vyote viwili wameishukuru Kamati ya Kudumu ya Bunge na wizara kwa kuwatembele na kusikiliza matatizo waliyonayo na wanaomani kuwa matatizo yao yatatafutiwa ufumbuzi.