KATIBU MKUU ADC DOYO ATOA USHAURI KWA RAIS SAMIA



Katibu Mkuu wa Chama cha Alliance Democratic Change (ADC) Doyo Hassan Doyo akizungumza katika kikao chake na baadhi ya wagombea wa nafasi mbalimbali za Ubunge na Udiwani kwenye uchaguzi mkuu uliopita alipokutana nao Jijini Tanga ikiwemo kuweka mikakati ya kujiimarisha zaidi kuelekea kwenye chaguzi zijazo

Katibu mkuu wa Chama cha Alliance Democratic Change (ADC) Doyo Hassan Doyo akiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kikao hicho


Katibu mkuu wa Chama cha Alliance Democratic Change (ADC) Doyo Hassan Doyo amemshauri Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kuhakikisha Serikali inapitia upya na kuziangalia tena kesi za uhujumu uchumi, utakatishaji wa fedha na kesi za ugaidi ambazo zinawakabili baadhi ya watanzania wanaoteseka magerezani kwa muda mrefu bila kupatikana ufumbuzi wake.

Hatua hiyo ya Katibu mkuu huyo inatokana na namna ambavyo Rais Samia alivyoonesha dhamira ya kupambana haki na wajibu basi aangalie vizuri sheria na ziweze kufanyiwa marekebisho lakini pia waliokamatwa na kuwekwa magerezani serikali iangalie namna ya kuzifuta kesi hizo ili watanzania waweze kunufaika na matunda ya nchi yao. 

Katibu Mkuu huyo alisema kwasababu watanzania wengi wanateseka kutokana na kesi walizopewa za uhujumu uchumi,  utakatishaji wa fedha na kesi za ugaidi kutokuwa na dhamana inapelekea watanzania wengi kuendelea kuteseka. 

Alisema kwa sababu Rais ameonyesha dhamira ya kupambana na kesi za namna hiyo basi kesi za namna hiyo ziangaliwe upya na ziweze kufutwa. 

"Watanzania wenzetu wanaendelea kuteseka na kesi hizo ambazo hazina dhamana kwasababu Rais ameonyesha nia ya kupambana basi aangalie namna ya kubadilisha hizi sheria zinazowakandamiza watanzania wenzetu kwanini tunatoa ushauri huu kwasababu tumemsikia Rais mwenyewe akisema kwamba Takukuru wamefuta kesi zaidi ya 140 za kubambikiza, "

Aliongeza kuwa hata hizi karibuni alipokuwa akifungua kiwanda cha polisi cha kushonea yunifomu akasema na  nyie jeshi la polisi angalieni angalieni kama kuna kesi za kubambika na nyie mzifute kwa kauli ya Rais ni mategemeo yetu kwamba hata hizi kesi zinazoitwa za uhujumu uchimi , utakatishaji wa fedha na kesi za ugaidi pengine nazo ni za kubambikiza. Alisisitiza Doyo. 

Alisema chama hicho wanaishauri Serikali kupitia Rais msikivu Samia Suluhu Hassan  kwenye majukumu na maamuzi mazito aweze kuwafikiria watanzania ili waweze kuishi nao kwa amani kama watu wengine wanavyoishi. 

"Unapopewa kesi ya uhujumu uchumi , utakatishaji wa fedha na kesi ya ugaidi kwa mujibu wa sheria zetu hazina dhamana na kitendo cha kumzuia mtu dhamana maana yake umwmnyima haki yake ya kikatiba ya msingi hivyo tunaomba sheria hizi ziweze kuangaliwa upya ili watanzania waweze kunufaika na matunda ya nchi yao.,"alisema Katibu Doyo. 

Awali akizungumzia dhamira ya ziara yake nchi nzima Katibu Doyo alisema ni kukutana na wanachama wao kuwapa pongezi kwa wale walioonyesha nia ya kuwania, nafasi mbalimbali katika uchaguzi mkuu uliopita na kuwapa pole kwa kimbunga walichokutana nacho katika uchaguzi huo lakini pia kuweka mikakati ya pamoja kuelekea kwenye uchaguzi wa serijali za mitaa. 
 
"Dhamaira ya kwanza ni kuja kutathimini kipigo cha uchaguzi mkuu uliopita lakini sasa tunajipanga kuelekea uchaguzi wa 2025 kwakuwa Rais aliyepo amesema uchaguzi ujao atakayepata amepata na atakayekosa amekosa ni tofauti na Rais aliyepita hivyo tulivyopata matumaini ya, mheshimiwa Rais sisi kama chama tumeona tuchukue hatua za kuweza kukutana na nyinyi kuwapongeza,  kuwapa pole lakini sasa tujipange na uchaguzi ujao tukiwa na matumaini ya kufanya vizuri, "alibainisha Doyo. 

Katibu Doyo alisema ameanza ziara tarehe 2 katika jiji la Daresalaam na wilaya zake zote,   Unguja na Pemba,  pamoja na Tanga ya kuongea na viongozi pamoja na watendaji na kubainisha kuwa ziara hiyo ni ya nchi nzima ambapo anaelekea Morogoro,  Singida, Dodoma,  Mwanza, Mara Simiyu,  Geita,  na Kigoma na mara baada ya hapo mapumziko mwezi ujao tarehe 15 wataendelea na ziara mikoa ya kusini kwa kusudio la kuinua uhai wa chama.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post