Na Queen Lema Arusha
Baraza la taifa la hifadhi na usimamizi wa mazingira limewataka wananchi kuongeza bidii kwenye kuongoa mifumo ya ikolojia
Hayo yamesemwa na Meneja wa nemc Kanda ya kaskazini Lewis nzali wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na siku ya mazingira duniani itakayo adhimishwa siku ya jumamosi
Amesema kuwa ili kuepuka athari zitokanazo na mifumo ikolojia wananchi wanapaswa kuongeza bidii kuongoa mifumo hiyo ili kuepuka Changamoto za mabadiliko ya tabia nchi
Amedai kuwa athari zitokanazo na mabadiliko ya tabia ya nchi ni kubwa sana na madhara yake ni makubwa hivyo basi jamii inatakiwa kuhakikisha tahadhari inachukuliwa
Katika hatua nyingine alidai kuwa baraza Hilo mkoa wa Arusha limeendelea kutoa elimu dhidi ya utunzaji na uboreshaji wa mazingira kwani mazingira yakiwa mabaya basi hata Uchumi nao hautastawi
"Mazingira ni pamoja na Uchumi mazingira yakiwa mabaya lazima kutakuwa na changamoto hivyo basi ni muhimu jamii ikatambua Hilo na ndio maana tunaendelea kutoa elimu"
Alihitimisha kwa kuwataka wananchi wahakikishe kuwa wanatunza mazingira pamoja na wawekezaji kuepuka kutiritisha maji machafu kwani wakibainika watachukuliwa hatua.