Mkuu wa Shughuli za Uwekaji Vinasaba Mhandisi Florian Batakanwa akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Shirika la Viwango (TBS) leo Jijini Dar es Salaam.
*********
SHIRIKA la Viwango Tanzania
(TBS),katika kipindi cha miezi miwili kasoro limefanikiwa kuweka
vinasaba katika lita Milioni 464,215,825 za mafuta na shughuli ya kuweka
vinasaba gharama yake kwa lita moja ni shilingi 14 hivyo mpaka sasa
wameweza kuingiza fedha kiasi cha shilingi Bilioni 6.5 na fedha hiyo
inaingia moja kwa moja serikalini.
Ameyasema hayo leo Mkuu wa
Shughuli za Uwekaji Vinasaba Mhandisi Florian Batakanwa akizungumza na
waandishi wa habari katika ofisi za Shirika la Viwango (TBS) leo Jijini
Dar es Salaam.
Amesema shughuli ya kuweka
vinasaba katika mafuta inawekwa kwenye maghara yanayopokea mafuta
bandarini ambayo kwa Dar es Salaam kuna maghala 19 ambayo wamekabidhiwa
na EWURA na mkoani kuna maghala matatu lakini pia kuna maghala mawili
yameongezeka hapa jijini na kufanya kufikia 21 kwa Dar es Salaam.
"Zoezi hili mwanzo lilikuwa
linafanywa na taasisi isiyo ya kiserikali hivyo mapato yote haya
yalikuwa yanaenda kwenye taasisi hiyo na serikali ilikuwa inapata kodi
kwenye taasisi hiyo'. Amesema Mhandisi Batakanwa.
Aidha Mhandisi Batakanwa amesema
hii zoezi la kuweka vinasaba kwenye mafuta lina uhusiano mkubwa na
usalama wa nchi kwani mtu ama kampuni binafsi akiweza kugawa vinasaba
kwa watu wasiohusika nchi inakuwa inateteleka kwasababu kiuchumi inakosa
mapato yake.