UNESCO yataka wanasayansi kushirikiana na jamii za asili kukabiliana na athari mabadiliko ya Tabia nchi.

 

Mwandishi wetu.


Arusha.Shirika la umoja wa Mataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) limewataka wataalam wa masuala ya Mazingira kuzisaidia Jamii za asili kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi kwa kutumia  utaalamu wa asili.


Afisa  wa UNESCO  wa masuala ya Mazingira na maarifa ya asili na Sayansi Dk. Nigel Crawhall alitoa wito huo wakati wa uzinduzi wa taarifa ya athari za mabadiliko ya Tabia nchi kwa Jamii za asili.


Dk Crawhall alisema jamii za asili zina maarifa ambayo yanaweza kusaidia kupunguza athari za mabadiliko ya Tabia nchi.


"Ni muhimu wanasayani kushirikiana na jamii hizi wamasai, Wahadzabe na wengine kujua utaalam wao na kuuboresha ili kupunguza athari za mabadiliko ya Tabia nchi"alisema


Mratibu wa mradi wa mabadiliko ya Tabia nchi katika shirika la PINGOs Forums, Gidioni Sanago alisema jamii za pembezoni   zimeathirika na mabadiliko ya tabia nchi hivyo muhimu kusaidiwa .


Sanago alisema hivi Sasa Mifugo imeanza kufa kwa kukosa malisho, migogoro ya ardhi imeongezeka lakini pia umasikini Kwa Jamii za asili unaongezeka.


Afisa jinsia wa shirika la PINGOs Forums,aNailejileji Tipap alisema wanawake wa jamii za asili ni waathiriwa wakubwa kwani wao ndio wanatembea muda mrefu kutafuta maji na malisho ya Mifugo.


Hata hivyo alisema wanawake wanaelimu ya asili ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi lakini bado hayatambuliwi na watungaji wa sera.


Adam ole Mwarabu alisema Jamii za asili zina elimu ya asili kupambana na mabadiliko ya tabia nchi lakini elimu na ujuzi wao hautambuliki hivyo wanasayansi na wadau wengine wanaweza kusaidia.


This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post