Serikali Njombe yatakiwa kusaka wanaotupa vichanga

 NJOMBE

Na Joctan Agustino

Kufuatia kukithiri kwa matukio ya kutupa na kutelekeza watoto katika kijiji cha Matiganjola kilichopo kata ya Ikuna wilayani Njombe ,Wakazi wa kata hiyo kutoka vijiji vya Nyombo na Matiganjola wameitaka serikali kufanya operesheni madhubuti ya kuwasaka wazazi wanaotelekeza watoto wao.

Imeelezwa kuwa wazazi wamekuwa wakifanya vitendo hivyo kwasababu mbalimbali zikiwemo za kiuchumi na migogoro ya kimahusiano na hivyo kushauri wanaotenda vitendo hivyo  kuchukuliwa hatua kali za kisheria dhidi yao ili kukomesha vitendo hivyo.

Wakizungumza katika mkutano wa hadhara wa mbunge wa jimbo la Lupembe wenye lengo la kusikiliza kero za wananchi na kueleza mipango ya maendeleo, wakazi wa vijiji vya Matiganjola na Nyombo akiwemo Michael Salingwa na Grace Nyagawa wamesema katika vijiji vyao kumekuwa na vitendo vya kujirudia vya kutupwa na kutelekezwa watoto hivyo wanaomba nguvu ya ziada ichukuliwa ya kukomesha vitendo hivyo vinahatarisha usalama wa taifa la kesho.

Mbali na watoto wakazi hao pia wamezungumzia changamoto ya ongezeko la tozo za mbao na mkaa na kwamba serikali ipunguze ili kunusuru tatizo la kukimbiwa na wanunuzi wa malighafi hizo.

Awali Mtendaji wa kata ya Ikuna Alestadia Naza na mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi ya chama cha mapinduzi wilaya ya Njombe Kasanga Makweta wanaswema kinachofanywa na baadhi ya wazazi kijiji hapo kina athari kubwa kwa vizazi vijavyo na kwamba chama hakitafumbia macho vitendo hivyo.

Nae mbunge wa jimbo la Lupembe Edwin Swalle akitolea ufafanuzi wa kero mbalimbali zilizowarishwa amesema kutupa mtoto kunapoka haki za msingi za mtoto ikiwemo ya kuishi na kuagiza kudhibitiwa mara moja huku pia akisema kuhusu suala la kero ya ongezeko la tozo za mbao na mkaa atazisemea katika vikao vya bunge.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post