TAMISEMI YAIPONGEZA DIT KWA MAFUNZO

 Kaimu Katibu Mkuu  kutoka Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Bw.Erick Kitali aipongeza DIT kwa kutoa mafunzo yatakayosaidia kutatua changamoto za Tehama kwa jamii.


Pongezi hizi amezitoa wakati akihitimsha  mafunzo ya kutengeneza 'photocopier' na 'printer'  kwa wataalam wa Tehama kutoka kwenye halmashauri nne na ofisi mbili za mikoa.



Alisema, "niipongeze DIT kupitia kituo cha Umahiri wa Tehama (ITCOITECT) kwa kutoa mafunzo haya muhimu yatakayosaidia kutatua changamoto ya muda mrefu iliyopo kwenye jamii kwa kuwa tunapokuwa na ubobezi wa ndani mambo yanafanyika vizuri ndani ya muda mfupi".



Nae Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) Prof.Preksedis Marco Ndomba ambae pia alishiriki kwenye hafla hii amesema kuwa, DIT inatekeleza agizo la Serikali la kuzitaka Taasisi za elimu kupambanua namna ya kuweza kutatua changamoto zilizopo kwenye jamii hivyo DIT inatekeleza hilo kupitia mafunzo kama haya yanayofanyika sasa.



Kwa upande wa  wanafunzi walionufaika na mafunzo hayo Bw. Innocent Sigred kutoka Kibaha Mji aliushukuru uongozi wa DIT kwa kuwa mafunzo waliyopata yatakuwa na manufaa kwao na ofisi wanakotoka kwani yatasaidia kuondoa gharama za utengenezaji wa vifaa na watatumia ujuzi huu kutengeneza vifaa vya ofisi.  

Mafunzo haya ya kutengeneza 'photocopier' na 'printer' yametolewa kwa siku 14 na kuhudhuriwa na wanafunzi saba (7) kutoka halmashauri ya Makete, kibaha,Meru,Ubungo na ofisi ya Mkuu wa mkoa Tanga na Geita.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post