Ajali ya moto yatokea Shinyanga, kamanda zimamoto atoa wito

 Na  Mapuli  Misalaba, Shinyanga

Kamanda wa Jeshi la zimamoto na uokoaji Mkoa wa Shinyanga GEORGE MRUTU ametoa wito kwa wananchi kutoa taarifa kwa wakati pale inapotokea majanga ya moto ili kuziwezesha mamlaka husika kufika kwa wakati.

Ametoa wito huo leo kufuatia ajari ya moto iliyotokea kwenye nyumba ya Bwana  Rashid Malunde mkazi wa mtaa wa Magadula kata ya Ngokolo katika Manispaa ya Shinyanga

Ajali hiyo ya moto imetokea leo majira ya saa nane mchana ambapo kwa mujibu wa watu wanaoishi katika nyumba hiyo wamesema hawakubaini mara moja chanzo cha moto huo

Kwa upande wake mwenyekiti wa mtaa huo Bwana HUMPHREY MTAFUNGWA amesema kwa ushirikiano mzuri wa wananchi wamefanikiwa kudhibiti moto huo kabla haujaleta madhara makubwa huku akieeleza namna alivyopokea taarifa za tukio hilo

“Hizi taarifa nimezipokea nusu saa iliyopita nimepigiwa simu kwamba katika mtaa wangu kunanyumba inaungua moto na mimi nikachukua jitihada za kufika hapa lakini bahati nzuri nimekuta wananchi wameudhibiti moto kwa kutumia maji ya bomba na vitu vingine vya kuzimia moto” ameongea Mtafungwa

Kufuatia ajali ya moto huo hakuna madhara yaliyotokea kwa binaadamu na kwamba tathimini ya vitu vilivyoungua haikupatikana mara moja wala Chanzo cha moto huo

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post