Fisi wa ajabu auawa,wananchi wanawaona kitoweo

 Na  Mapuli  Misalaba,  Shinyanga

Katika hali isiyokuwa ya kawaida baadhi ya wananchi wameshiriki kumuua mnyama anaye sadikika kuwa ni fisi katika eneo la mto mumbu matanda mtaa wa Chamaguha Manispaa ya Shinyanga na  kugawanaviungo vyake ikiwemo damu,miguu,kichwa, ngozi na kisha kuondoka navyo  kwa sababu zisizojulikana 

Baadhi ya watu walioshuhudia tukio hilo wamesema fisi huyo amegongwa na gari majira ya sa 1.00 asubuhi na kushindwa kutembea baada ya kuvunjika miguu yake ya mbele hali iliyomlazimu aingie kwenye mtaro wa barabara kwa lengo la kujificha kabla ya kuuawa na wanachi

Mwenyekiti wa mtaa huo HUSSEN KATAMBA amewatahadharisha wananchi kuwa makini hasa kwa watoto kutokana na wanyama aina ya fisi kuonekana katika maeneo mbalimbali ya Manispaa ya Shinyanga

Amesema wanyama hao tayari wamesababisha madhara katika baadhi ya maeneo hivyo wazazi wanapaswa kuwalinda watoto

“Natoa tahadhari hasa  sisi wazazi tusiwaluhusu watoto kutembea asubuhi sana au usimu kumtuma dukani  tuwe makini kwa sababu hatujui huyo fisi atatokea lini na sangapi hasa kwa maeneo ya chamaguha kwa sababu siyo mara ya kwanza kuonekana fisi kwahiyo nawaomba sana wazazi tuchukue tahadhari hiyo” amesema Katamba

Aidha ameiomba serikali kupitia viongozi wa mali ya siri kutafuta njia ya kuwapata hao wanyama kabla hawajaleta madhara kwa wananchi hasa watoto

“Tunasikia kwenye vyombo vya habari fisi wanajeruhi watu na kusababisha vifo na kama wanaendelea kuonekana namna hii itabidi wahusika hasa mali ya siri wajaribu kuwasaka ili kujua wanakaa wapi kwa sababu hili eneo hatuna msitu sasa tunajiuliza hawa fisi wanakaa wapi”

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post