Madiwani tisa Tanga wapewa ramani za kidijitali *Zitasaidia kuboresha mazingira Mkoa wa Tanga

 

Na Mwandishi Wetu, Tanga

KATA tisa za Mkoa wa Tanga zimepokea ramani za kidigitali zinazoonesha taarifa za maeneo na mifumo taarifa za kijografia (GIS) ili kusaidia katika kuboresha huduma za ukusanyaji taka ngumu na utambuzi wa maeneo hatarishi kiafya na kiusalama.


Baadhi ya wadau walioshiriki mkutano wa kuboresha taarifa na takwimu zilizokusanywa na wanafunzi wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU), na vijana wa Mkoa wa Tanga kwenye mradi wa Livinglab unaoendeshwa kwa pamoja na Tanzania Daba Lab, Jiji la Tanga na ARU kwaaajili ya kuboresha mazingira ya Mkoa huo.


Mkurugenzi wa Tanzania Data Lab, Stephen Chacha, akifafanua jambo wakati wa mkutano na madiwani na wadau mbalimbali uliohusu kuboresha taarifa zilizokusanywa na wanafunzi wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU) kwa kushirikiana na vijana wa Tanga kwenye mradi wa Livinglab unaoendeshwa na Jiji la Tanga, ARU na Tanzania Data Lab kwaajili ya kuboresha Jiji la Tanga
Naibu Meya wa Jiji la Tanga, Joseph Colyvas (kulia) akiwa ameshika ramani ya kidigitali yenye taarifa za kijografia kwenye kata zao akiwa na madiwani wenzake wa Tanga waliyokabidhiwa kwenye mradi wa Livinglab  unaoendeshwa na Tanzania Data Lab, Chuo Kikuu Ardhi (ARU) na Jiji la Tanga unaofadhiliwa na Foundation Botnar ya Uswisi.

Ramani hizo pia zinaonyesha taarifa za maeneo muhimu, mitaa na majengo pamoja na mifumo ya kusimamia mipango ya maendeleo ya Jiji la Tanga.

 Kata hizo ni pamoja na kata ya Chumbageni, Central, Ngamiani Kaskazini, Ngamiani Kusini na Ngamiani Kati. Zingine ni Majengo, Usagara, Duga na Nguvumali.

Mkurugenzi wa Tanzania Data Lab Stephen Chacha, alisema kuwa mradi huo wa LivingLab Initiative una lengo la kuwezesha matumizi ya data kufanya maamuzi mkoani Tanga.

Alisema mradi huo wa Livinglab unatatajiwa kulifanya Jiji hilo kuwa la kimataifa kwa usafi na kwa mpangilio wake na madi huo wa miaka mitatu unatekelezwa kwa pamoja na Halmashauri ya Jiji la Tanga, Chuo Kikuu Ardhi na Tanzania Data Lab kwa ufadhili wa Fondation Botnar ya Uswis.

Alisema mbali na kulipaisha Jiji hilo kimataifa, pia unatarajiwa kuibua fursa mbalimbali za kiuchumi kwa vijana wa mkoa huo ambao wamekuwa wakishirikishwa kila hatua ya mradi huo.

Akizungumza kwenye mkutano huo uliowashirikisha madiwani na watendaji wa wa Jiji hilo, Chacha alisema vijana waliotumika kukusanya taarifa na takwimu hizo ni kutoka Chuo Kikuu Ardhi (ARU) na vijana wa Mkoa wa Tanga.


Alisema vijana hao wamefanyakazi kubwa kwa ufanisi wa hali ya juu kuibua fursa mbalimbali za Mkoa wa Tanga na kutoa takwimu na taarifa ambazo zitakuwa msaada mkubwa kwenye mipango miji.

Alisema kabla ya kuanza kwa mradi huo Jiji la Tanga lilikuwa katika hali mbaya kimpangilio lakini baada ya mradi huo mtu anaweza kutafuta mtaa na taarifa mbalimbali za Mkoa huo kiganjani mwake.

" Sasa hivi unaweza ukaingia kwenye simu yako ukatafuta taarifa mbalimbali za Mkoa wa Tanga, mitaa imeanishwa na kila nyumba na inatumika kwa biashara gani viko mtandaoni," alisema.


Naibu Meya wa Jiji la Tanga, Joseph Colyvas alisema mradi huo ni muhimu kwani umeliweka Jiji la Tanga kwenye ramani ya dunia.

Alisema mradi huo umeibua mambo mengi zikiweno sehemu ambazo si salama, maeneo ya wazi, na maeneo ya utupaji taka. Hali hii itasaidia sana hata kupunguza migogoro ya ardhi.

"Botnar wametuambia leo kwamba kuna bilioni 7 zinatarajiwa kuletwa kwaajili ya maendeleo  ya Tanga. Tunawashukuru sana kwani hadhi ya Jiji letu itapaa na pengine kuyapita majiji mengine,” alisema Naibu Meya.

" Tumemwelekeza mtu wetu wa IT kwamba hizi takwimu na taarifa aziweke kwenye kanzidata yetu maana zitatusaidia sana kupata hata wawekezaji,” alisema

Aidha,  Naibu Meya huyo aliwaomba madiwani na watendaji wa Jiji la Tanga kuhakikisha wanashirikiana kutekeleza miradi inayofadhiliwa na Botnar ili wasioneoke nchini. Aliwaomba wawakilishi wa Fondation  Botnar kuandaa mafunzo zaidi hata kwa madiwani ambayo kata zao hazijapitiwa na mradi huo ili waweze wawe na uelewa wa pamoja kuhusu mradi huo.

Mwanafunzi wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU)Happy William aliyeshiriki kukusanya data alisema mbali na kumwongezea maarifa mradi huo umemwezeaha kujua namna teknolojia inavyoweza kutatua mambo mbalimbali.

Mwanafunzi mwingine wa ARU,  anayesomea upangaji wa makazi na miundombinu, Rasi Mbwana alisema  amepata fursa ya kujua fursa mbalimbali zinazopatikana mkoa wa Tanga

"Nimejifunza na kupata uzoefu wa kutumia teknolojia ya habari na mawasiliano ( ICT) kutatua changamoto mbalimbali  na mradi utatatua changamoto za vijana kama matumizi ya dawa za kulevya kwa kuwapatia fursa za ajira, " alisema

Alisema miongoni mwa masuala yaliyoibuliwa na mradi huo ni maeneo ambayo kuna mbu wengi wanaosabisha ongezeko la Malaria

Mwakilishi wa Foundation Botnar nchini Tanzania, Dk. Hassan Mshinda akizungumza kwenye mkutano wa mkutano wa kuboresha taarifa na takwimu zilizokusanywa na wanafunzi wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU), na vijana wa Mkoa wa Tanga kwenye mradi wa Livinglab unaoendeshwa kwa pamoja na Tanzania Daba Lab, Jiji la Tanga na ARU kwaaajili ya kuboresha mazingira ya Mkoa huo.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post