Mtu mmoja afariki dunia na saba kujeruhiwa katika ajali ya gari Tinde Shinyanga

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga George Kyando

 Na  Mapuli  Misalaba,  Shinyanga

Mtu mmoja amefariki dunia na wengine saba kujeruhiwa kufuatia ajali ya Gari aliyokuwa amepanda kuligonga trekta kwenye eneo la kijiji cha Ishinabulandi kata ya Samuye Barabara ya tinde-Tabora.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga kamishina msaidizi wa Polisi GEORGE KYANDO amesema ajali hiyo imetokea jana   saa 2,30 usiku katika kijiji hicho.

Amesemag garihiyo aina ya Toyota HICE yenye namba za usajili T470 DEL iliigonga trekta lenye namba  T623 CKY  na kusababisha kifo cha abiria huyo na majeruhi saba.

Gari hiyo ambayo ni mali ya kampuni ya kisimbo and sons limited ilikuwa ikiendeshwa na Sudi Ntawigaya  25,mkazi wa Ibinzamata wakati trekta ilikuwa ikiendeshwa na na Shija Steven mkazi wa Ishinabulandi 

Kamanda kyando amewataja majeruhi hao kuwa ni Shija Deus, Mohamed Juma, wote hao ni wakazi wa Ishinabulandi Venence Jonas mkazi wa Ndala, Maneno Charles mkazi wa Kitangili wengine ni Paulo Stephano ambaye hakufahamika mara moja makazi yake, Shabani Moharmed mkazi wa Majengo mapya pamoja na Josia Magabe mkazi wa Kitangili katika Manispaa ya Shinyanga 

Chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa HICE kutaka kuyapita magari mengine kwa mwendo hatarishi na kwamba jeshi la polisi linaendelea kumtafuta dereva huyo ambaye ametoroka baada ya kutokea kwa ajali  hiyo

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post