Wagombea wa CCM, ACT kuchuana nafasi ya udiwani Shinyanga, tisa waenguliwa kwa kukosa sifa

Victor Mmanywa, mgombea wa CCM

 Na  Mapuli  Misalaba,  Shinyanga

Zoezi la kuchukua na kurudisha fomu za kuwania nafasi ya udiwani katika uchaguzi mdogo kata ya Ndembezi limehitimishwa leo ambapo wagombea wawili kati ya 11 waliochukua fomu wameteuliwa kuviwakilisha vyama vyao kwenye kinyang’anyiro hicho.

MVANO ABDUL IDD wa chama cha ACT wazalendo 
Msimamizi msaidizi wa uchaguzi kata ya Ndembezi Bwana TIMOTHY ANDREW TIMOTHY

Msimamizi msaidizi wa uchaguzi kata ya Ndembezi TIMOTHY ANDREW TIMOTHY amewataja walioteuliwa  kuwa ni MVANO ABDUL IDD wa chama cha ACT wazalendo na VICTOR TOBIAS MMANYWA wa chama cha mapinduzi CCM,baada ya kukidhi matakwa ya kikanuni ya tume ya uchaguzi ikiwemo kuchukua na kurudisha fomu kwa wakati uliopangwa 

Afisa huyo amevitaja vyama tisa  ambavyo wagombea wake hawakufanikiwa kurudisha fomu 

“Bwana Abdallah Sube wa Chama cha Demokrasia Makini,Rehema Mjengi (ACD), Antony Ndida (SAU), Ramla Shija (NLD), Fatuma Ally (UMD), Emiliana Malema CCK, Ibrahim juma (CHAUMA), Lwitakubi Kabugulu (NRA), Amen Isangi (DP)

Msimamizi huyo wa uchaguzi amesema hatua inayofuata baada ya uteuzi wa majina ya wagombea ni wananchi kuweka pingamizi zoezi ambalo litahitimishwa kesho saa kumi ili kuruhusu hatua nyingine za mchakato wa uchaguzi kuendelea 

Aidha Timothy amesema kikao kilichowateua ni kikao cha wasimamizi wa uchaguzi ambapo ametoa wito kwa wananchi kwa yeyote mwenye pingamizi juu ya hao walioteuliwa ofisi ziko wazi ndani ya muda uliopangwa.

Mchakato huo wa uchaguzi unafuatia aliyekuwa Diwani wa kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga David Nkulila kufariki Dunia siku za hivi karibuni ambaye pia alikuwa meya wa Manispaa ya Shinyanga.



This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post