MARIA MAKOMBE ALETA TEKNOLOJIA MPYA YA UFUGAJI SAMAKI KWA VIZIMBA BWAWA LA NZIVI MUFINDI

 


Uwekezaji mkubwa wa ufugaji samaki Kwa njia ya vizimba imetajwa kuwa ni fursa kubwa ya uwekezaji Katika bwawa la Nzivi wilaya ya Mufindi mkoani Iringa .


Hatua ya uwekezaji huo mkubwa unekuja huku Serikali ya mkoa wa Iringa chini ya mkuu wa mkoa  Queen Sendiga imeendelea kuhamasisha wananchi wa mkoa huo kuwekeza Katika mabwawa ya Samaki na Kilimo cha Parachichi.


Akimzungumzia juu ya uwekezaji huo unaendelea bwawa la Nzivi Mufindi Mjasiriamali Maria Makombe amesema kuwa ufugaji wa kizimba ama vizimba umekuwa ukifanyika Katika  Ziwa ama mabwawa na umekuwa na manufaa makubwa Sana.



Amezitaja faida kubwa Katika ufugaki wa  vizimba  kuwa ni 

Kukuza biashara ya samaki kwa kiasi kikubwa,

Kutengeneza ajira kwa wauzaji wa samaki maana kwa kutumia vizimba pindi unapoanza kuvuna unavuna samaki wengi kwa wakati mmoja.


Pia kukuza uchumi wa eneo husika maana vizimba vinavutia watu wengi kuwekeza hivyo sehemu husika lazima itafaidika na ajira na mapato pia.



Aidha ufugaji huo ni sehemu ya utalii Kwa wilaya ya Mufindi na mkoa wa Iringa maana hakuna sehemu ndani ya mkoa wa Iringa ufugaji huo unafanyika wakati Kuna mabwawa mengi zaidi .


Maria amesema kuwa wanawake wanapaswa kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan Kwa kufanya shughuli za ujasiriamali kama hizo kupitia rasrimali zinazowazunguka Kwa Ardhi ,mito na nyingine nyingi .


Kuwa iwapo wanawake wataunga mkono jitihada hizo za Rais Kwa kufanya kazi ni wazi maendeleo yataonekana na kweli azma ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kazi iendelee itafanikiwa Kwa kila mmoja wetu .

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post