Na Queen Lema Arusha
Westerwelle Foundation kutoka Ujerumani imeungana na Obuntu Hub kutoka Tanzania kufungua kituo kipya kwa ajili ya kuwainua vijana wajasiriamali yaani Innovation Hub
Mbali na kufungua kituo hicho Jijini Arusha pia mpaka sasa vijana Zaidi ya 200 wameshanufaika na kituo hicho
Akiongea mwishoni mwa wiki na waandishi wa habari mara baada ya kufungua kituo hicho,Meneja mkuu wa Westerwelle Startup Haus Arusha Bw Collins Kimaro alisema kuwa uwepo wa kituo hicho ni msaada mkubwa sana kwa vijana
Kimaro alisema kuwa vijana hao 200 walipatiwa ujuzi wa kidigitali kutoka katika sekta ya kilimo
Kimaro alisema kuwa vijana hao kutoka Arusha na Iringa walipewa ujuzi wa kidigitali
"Ni fursa kubwa sasa kwa vijana kunufaika na kituo hiki maana hata hao vijana 200 ambao tumewafikia toka mwezi June tayari matokeo yameshaonekana kwaiyo tuseme kuwa kila kijana mjasiriamali sasa atumie kituo hiki"aliongeza
Akiongea kituo hicho alisema kuwa ni muungano wa Obuntu Hub na Westerwelle Foundation,ambapo sasa kwa umoja huo wamefungua Westerwelle Startup Haus Arusha(WSHA) ambapo kituo hicho kitatoa nafasi za kisasa za kufanyia kazi yaani co working space,
Aliongeza kuwa programu ya mafunzo mbalimbali na kuwakutanisha wajasiriamali wa kitanzania na mtandao kimataifa
Kimaro alibainisha kuwa anawashukuru wafadhili mbalimbali ambao wamejitolea kuwasaidia vijana ambapo mpaka sasa matunda yameshaonekana
Alihitimisha kwa kusema kuwa kwa sasa vijana wanakabiliwa na changamoto Kama vile ukosefu wa mitaji,na masoko lakini sasa wanatakiwa kujiunga na kituo hicho,lakini pia wanatakiwa kuchangamkia fursa pamoja na mashindano ya kimataifa ambayo yanatangazwa.
Naye mkurugenzi wa Westerwelle foundation Bw Oliver Reisner alisema kuwa limefurai sana kufika Tanzania na wameona muamko wa vijana na wataungana na jitiada za Serikali ya Tanzania kuchochea maendeleo kupitia ubunifu na ujasiriamali.
George Akilimali ni mmoja wa wanufaika,alisema kuwa umoja huo umekuwa msaada kwa vijana wengi sana hapa nchini ambapo kwa yeye aliweza kupata msaada mbalimbali ikiwemo elimu,na mtaji
Alidai kuwa hapo awali hakuwa na uwezo wa kupata masoko ya kimataifa ila kwa sasa amekutanishwa na wadau wa kimataifa hivyo vijana wanatakiwa kutumia kituo hicho
Wadau mbalimbali wa Westerwelle Startup Haus Arusha wakijadili jambo wiki iliyopita kwenye uzinduzi wa kituo hicho Jijini Arusha,picha na Queen Lema |
Mkurugenzi wa Westerwelle foundation Bw Oliver Reisner akiteta jambo wakati wa uzinduzi wa kituo hicho jijini Arusha |