Imarisheni ulinzi wa mtoto, hali ni mbaya: RC Shinyanga

 Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Serikali Mkoani Shinyanga imeendelea kuwaomba washirika wake katika mapambano ya kupinga ukatili wa kijinsia kwa Watoto, kuwekeza zaidi  kwenye  ulinzi na usalama wa Mtoto ili kuwa na Taifa lenye watoto wanaoishi katika mazingira salama.


Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga kwenye kilele cha Maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika, Mgeni rasmi katibu tawala wa Wilaya ya Shinyanga Boniface Chambi,  amewaomba wadau wote yakiwemo mashirika yasiyo ya kiserikali,asasi za kiraia,taasisi na Watu binafsi,viongozi wa dini pamoja na Wazazi na walezi kuendelea kukemea vitendo vya ukatili dhidi ya Watoto, ili kupunguza matukio hayo.


Katibu tawala wa Wilaya ya Shinyanga bwana Chambi amewasisitiza wazazi na walezi wa watoto kuhakikisha wanatimiza wajibu wao kwa kuzingatia haki za mtoto ikiwemo haki ya kulindwa, kupata elimu, chakula pamoja na mavazi bora.


Amesema serikali ya Mkoa wa Shinyanga itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wanaopinga ukatili kwenye jamii ili kuhakikisha mkoa unaendelea kuwa salama dhidi ya vitendo vya ukatili.


''Leo tunaadhimisha siku ya mtoto wa afrika huku tukitambua kuwa baadhi ya watoto nimathura wa ubakaji, ulawiti na vipigo ambavyo kwa kiasi kikubwa vitendo hivi vinafanywa na watu wa karibu sana wakiwemo baba, mama, bibi na wengine katika hali isiyotegemewa vitendo vya ukatili vimekuwa vikijitokeza shuleni na katika taasisi za Dini hali ambayo inapoteza zaidi usalama wa watoto wetu matukio haya ni lazima tuyakemee kwa pamoja''


''Natoa rai kwa wazazi, walezi, viongozi wa dini, viongozi wa serikali na kila mwana jamii kutoa kipaumbele cha kwanza katika  ulinzi wa mtoto kwani hao ni Taifa la kesho tukishindwa kuweka msingi mzuri wa malezi kwa watoto wetu tutahatarisha ulinzi wa Nchi yetu sisi sote tunapaswa kuhakikisha watoto wetu wanalindwa, wanapata mavazi, chakula, maradhi bora na kupata elimu''. amesema katibu tawala Chambi.


Akizungumza kwa niaba ya afisa ustawi wa Mkoa wa Shinyanga, afisa ustawi wa Hospital ya rufaa Mkoa wa Shinyanga Prisla Mushi ametaja takwimu ya ukatili katika kipindi cha Julai 2021 hadi Mei 2022 ambapo jumla ya matukio ya ukatili wa watoto kwa Mkoa wa Shinyanga ni 4660.


''Kwa wasichana  ni 3313 wakiwemo wavulana 1341 lakini pia pamoja na hiyo takwimu kuna takwimu fupi ya mimba za utotoni kwa kipindi cha Julai 2021 mpaka Mei 2022 ni 166 na ndoa za utotoni katika kipindi hicho hicho cha Julai 2021 hadi Mei 2022 wako 61'' ametaja afisa ustawi Mushi.


Naye mkuu wa dawati la jinsia na watoto Polisi Wilaya ya Shinyanga Blighton Rutajama John amesema  kufuatia tukio la ukatili dhidi ya  watoto wawili katika kata ya Lyabukande Wilaya ya Shinyanga, hali ambayo  ilisababisha  kifo na majeruhi Waziri wa Maendeleo ya jamii, jinsia,wanawake na makundi maalum Dokta Doroth Gwajima alifika katika eneo hilo na kutoa maelekezo kuwa taratibu za kisheria zichukuliwe kwa watuhumiwa.


Mkuu wa dawati la jinsia na watoto Polisi Wilaya ya Shinyanga  Rutajama amesema maelekezo ya waziri Dkt. Gwajibu yametekelezwa baada ya Jeshi hilo kufanya upelelezi tayari watuhumiwa wapo mahakamani.


April  18, Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga lilitoa taarifa za  kuuawa kwa Mtoto Joseph Juma mwenye umri wa Miaka minne, Mkazi wa kijiji na kata ya Lyabukande katika halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, ambaye alipigwa na Bibi yake sehemu mbalimbali za mwili wake kisha kumwagiwa maji ya moto hali iliyomsababishia kifo chake. 


Aidha katika kilele cha maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika yaliyofanyika kimkoa katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga baadhi ya Watoto wameomba juhudi zaidi kuendelea kuwekezwa kwenye ulinzi na usalama wa Mtoto.


Kilele cha siku ya Mtoto wa Afrika kimkoa  yamefanyika katika kata ya Lyabukande Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga,ambapo kauli mbiu yake inasema "Tuimarishe ulinzi wa mtoto, Tokomeza ukatili dhidi yake, tujiandae kuhesabiwa."

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post