JESHI LA POLISI :ACHENI KUGEUZA MAGARI YA WANAFUNZI KUWA KICHAKA CHA KUHIFADHIA MAGARI MABOVU

 

Baadhi ya magari yaliyokutwa na makosa mbalimbali ambapo yaling'olewa namba hadi pale watakaporekebisha makosa hayo.Picha na Vero Ignatus.
Baadhi yaMagari ya kubebea wanafunzi yakiwa kwenye foleni kwaajili ya ukaguzi mbalimbali Chini ukaguzi wa Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama barabarani Mkoani Arusha
Baadhi yaMagari ya kubebea wanafunzi yakiwa kwenye foleni kwaajili ya ukaguzi mbalimbali Chini ukaguzi wa Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama barabarani Mkoani Arusha
Mrakibu wa Polisi na Mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani mkoa wa Arusha Solomoni Mwangamilo  akizungumza na baadhi ya madereva wa magari ya kubeba wanafunzi kwa shule binafsi Jijini Arusha.Picha na Vero Ignatus.  
Baadhi ya magari yaliyokutwa na makosa mbalimbali yakiwa yameng'olewa namba hadimpale wamiliki wao watakaporekebisha makosa hayo .Picha na Vero Ignatus.


Na.Vero Ignatus,Arusha

Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama barabarani kimeendesha zoezi mahususi kwa ukaguzi wa vyombo vya moto wakiwa wamejikita kwenye magari yanayobeba wanafunzi,ambapo magari zaidi ya 163 yamekaguliwa huku magari 17 yakiondolewa namba zake za usajili kutokana na kukutwa na makosa mbalimbali.

Mrakibu wa Polisi na Mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani mkoa wa Arusha Solomoni Mwangamilo  akizungumza na Michuzi Blog, amewataka wamiliki wote wenye magari ya shule kuyapeleke vituo vilivyoainishwa kwaajili ya ukaguzi kwani msako utaanza siku ya jumatatu kwa magari yote ambayo hayana hati ya ukaguzi ambapo hatua stahiki itachukuliwa

 Mwangamilo amesema kuwa Jeshi la polisi mbali na kuangalia usalama wa rai na mali zao pia wamejikita kwenye ‘’Usalama wa mtoto’’hivyo hawataruhusu kuona magari ambayo hayajakaguliwa kuwa barabarani,kwani baadhi  yamefanywa kuwa  kama kichaka cha kuhifadhia magari mabovu

‘’Magari haya hayaridhishi katika ubora wake sasa lengo letu sisi ni kuhakikisha kuwa kila chombo kinapokuwa barabarani kiwe kimekidhi vigezo sasa haya magari ya shule, mengi yamefanywa ni kichaka cha kuhifadhia magari mabovu, yaani mmiliki akishindwa ushindani wa kazi za daladala kutokana na hali ya gari yake imekuwa siyo nzuri sana anaikimbiza kwenda kubebea wanafunzi ,huku wakiamini kuwa hatuyakaguliwi mara kwa mara kwa kutokuharibu ratiba ya wanafunzi‘’Amesema Mwangamilo

Mwangamilo amesema awali waliwaandikia wamiliki wa shule hizo na kuwataka kupeleka  idadi ya magari ,ila hadi ukaguzi unaanza bado siyo wamiliki wote wamekuwa waaminifu kutimiza agizo hilo,bali inaonekana upo ujanja unaotendeka kwa kuchagua magari yenye hali nzuri na kuyapeleka,baliJeshi la polisi limesema wao wametimiza jukumu la kuyakagua magari hayo.

‘’Shule zina magari mengi bado hayajafikia kiwango ambacho kipo katika magari ya shule ,ninachokiona hapa kuna ujanja ujanja unatendeka kwa kuchagua magari yenye hali nzuri ndiyo wameyaleta,sisi tunayakagua kutokana na viwango vyetu,ila niwaambie wamiliki wa shule kuna magari ambayo wameyaficha hawataki kuyaleta kwaajili ya uchaguzi] na wapate ushauri wa kiufundi’’

Aidha amesisisitiza kuwa ukaguzi huo ni wa lazima kutoka ndani ya jeshi la polisi,hivyo endapo watashindwa kufuata maelekezo  yaliyotolewa na jeshi hilo, magari hayo kuanzia siku ya jumatatu 13 juni 2022,wataanza oparesheni katika kila eneo  kuhakikisha kwamba yale magari ambayo hayana hati ya ukaguzi yanakamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria

‘’Hatua hizi zinaweza kwenda mbali sana hata mmiliki wa gari hilo anaweza kuchukuliwa hatua  ,na gari yeyote ambayo itakutwa haina ripoti ya ukaguzi itapelekea sisi kutambua kuwa lilikuwa gari limefichwa wakati yalipohitajika kwa ukaguzi.

Aidha ukaguzi huo wa siku mbili wa magari ya kubeba wanafunzi (school bus)umeanza leo jumamosi utamalizika siku ya kesho jumapili 12juni 2022 ili kutokuvuruga utaratibu wa wanafunzi,unaendelea katika halmashauri ya Jiji la Arusha,arusha Dc,Arumeru na Longido .



This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post