KKKT yafanikiwa kumaliza deni la Bil12

Kanisa la kkkt dayosisi ya Kaskazini kati limefanikiwa kumaliza deni la kiasi cha zaidi ya  Bilioni 12 ambazo zilikuwa zinadaiwa na benki ya Crdb  kwa ajili ya Hoteli ya  Corridor Springs iliopo jijini Arusha 

Akiongea Jana na vyombo vya habari mara baada ya kumalizika kwa ibada maalumu ya shukurani iliofanyika katika usharika wa Kimandolu jijini hapa Askofu wa dayosisi hiyo Dkt Solomoni Masangwa alisema kuwa hatua waliofika ni njema na wameweza kumaliza kabisa deni hilo.


Akiongea chanzo halisi cha deni hilo alidai kuwa Tangu mkopo huo ulipochukuliwa mwaka 2007 hadi mwaka 2011 marejesho ya mkopo hayakufanyika hivyo kulikimbikiza mkopo na riba hadi kufikia Dola Milioni 4,712769 sawa na Tsh Bilioni 8.73 ikiwa pamoja na ongezeko la Dola 1,212769 sawa na Tsh Bilioni 2.24


Aliongeza kuwa hata baada ya hapo bado Hoteli iliendelea kushindwa kurejesha  mkopo huo,hivyo Dayosisi ikaanzisha mazungumzo na benki hiyo ili mkopo huo uweze kufanyiwa marekebisho ambapo marekebisho ya mkataba  yalifanyika May 3 mwaka 2011


Dkt Masangwa alidai kuwa baada ya marekebisho Dayosisi ilianzisha mchakato wa kukusanya fedha kwa kutumia mkakati mbalimbali ili kumaliza deni hilo.


Askofu huyo alitaja mikakati hiyo kuwa ni pamoja na mkopo toka kwa waumini wa dayosisi hiyo ambapo watu 4 walijitokeza na walichanga Tsh Milioni 110.


Mkakati mwingine alioutaja ni mikopo toka baadhi ya sharika, ambapo mkakati huo haukufanikiwa, huku mkakati mwingine kuwa na  siku 4 kwa kila mwaka kutoa sadaka ya kurejesha mkopo ingawaje napo hawakufanikiwa 


Alitaja mkakati mwingine ambao wao Kama Dayosisi walijaribu kuutumia kuwa ni pamoja na kuwachangisha waumini  wa dayosisi hiyo  wapatao 50,000 kila mmoja kutoa 20,000 lengo likiwa ni kupata kiasi cha Bilioni 1 ambapo kiasi kilichopatikana ni Milioni 12.85 zikiwa ni chini ya lengo  la shilingi Milioni987.15 na fedha hizo hazikuweza kupunguza deni hilo ambalo liliendelea kuongezeka 


Kutokana na hali hiyo alisema kuwa Dayosisi iliitisha kikao mwaka 2015 cha mazungumzo na benki hiyo ili kuomba mkopo ufanyiwe marekebisho tena ambapo kwa wakati huo mkopo  Dola mil6,136,580 sawa na Tsh Bilioni 11.4 ambapo riba ya kila siku ilikuwa ni Dola 1,403 sawa na Tsh Milioni 2.6 na benki hiyo ilitaka Dayosisi iandae mchakato wa namna Hoteli hiyo itakavyolipa deni hilo.


"Kikao hicho kiliazimia mambo mbalimbali ambapo CRDB walitoa sharti la kulipa sh Bilioni 2.5 ifikapo julai 31 mwaka 2015 ili mkataba uweze kusainiwa,malipo yalilipwa na mkataba ukasainiwa.


Tulianza kulipa mkopo pamoja na riba kuanzia January 2017 kiasi cha tsh Milioni 68,639,701 na baada ya hapo  kamati ilianza kazi ya kubuni mbinu mbalimbali za kupata fedha  kwa ajili ya kulipa marejesho ya kila mwezi pamoja na fedha za malipo ya awali sh Bilioni 2.5


Mbinu ambazo zilitumika kupata fedha ni kuweka uwiano kwa kila usharika kuchangia,kufanya uwekezaji wa fedha za makusanyo na kupata riba,uwekaji kwenye hati fungani za benki kuu(Bot)iliingiza faida iliyopatikana kiasi cha shilingi 865,271,400hivyo uwekezaji mzima ulizaa Tsh 1,044,645,126 na uwekezaji huo uliwezesha kujaza mapungufu ya michango na kuwezesha kukamilika malipo ya mkopo January 31 2022ikiwa ni miaka miwili na miezi11 kqbla ya muda uliopangwa"alidai Dkt Masangwa


Akiongelea hali ya Hoteli kwa sasa alisema kuwa mapato yameongezeka kutoka sh 459 Milioni kwa mwaka 2015 hadi kufikia sh Bilioni 1.259 kwa mwaka 2021 sawa na ongezeko la asilimia 274 ingawaje kulikuwa na wimbi la ugonjwa wa Corona


"Wageni sasa wameongezeka sana tena sana kutoka 5912 mwaka 2015 mpaka 21694 mwaka 2021 sawa na ongezeko la asilimia 367 na kwa sasa Hoteli ina uwezo wa kujiendesha yenyewe huku Hoteli ikiwa imepanda na kuwa ya hadhi ya nyota tatu"aliongeza 


Alisema wanashukuru wadau na washarika, benki hiyo ya Crdb kwa kuungana na Kisha kufuta deni hilo

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post