Mbarawa kufungua kongamano la uchumi wa bluu


Na Mwandishi Wetu

CHUO cha Bahari (DMI), kimewataka watanzania kuchangamkia fursa ya mafunzo ya fani ya ubaharia kutokana na kuwa na soko kubwa la ajira nchini na kwenye mataifa mbalimbali duniani.



Wito huo ulitolewa jana jijini Dar es Salaam na Kaimu Mkuu wa chuo hicho, Tumaini Gurumo, wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini.



 Alikuwa akizungumzia mkutano wa mabaharia kongamano la kwanza ala uchumi wa bluu leo na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa litakalohudhuriwa na mabalozi wan chi mbalimbali zenye bahari.



Alisema ubaharia ni fani kama zilivyo fani zingine zenye heshima ambayo husomewa kwa vitendo na nadharia na hatimaye akifaulu anapata cheti na kupanda madaraja kama ilivyo kwa fani ziingine.



Alisema mafunzo yanayotolewa na DMI yana ithibati ya kimataifa na baharia anayefundishwa na chuo hicho anauwezo wa kufanya kazi ndani ya nchi na kwingine kote duniani kwani vyeti vyake vitakauwa vinatambuliwa kimataifa.



“Uhitaji wa mabaharia duniani bado ni mkubwa sana wanahitajika wengi sana nan chi nyingi zina meli lakini hazina watu na Ukraine ilikuwa inatoa mabaharia wengi sana lakini katika kipindi hiki cha vita hakuna mabaharia wengi wa huko wako nyumbani hivyo nafasi inazidi kuongezeka kwa mabaharia wa kitanzania.



“Kuna fursa kubwa sana kwenye fani ya ubaharia nawaasa vijana, wazazi na walezi waitazame, fani hii zamani ilionekana kama vile ya kihuni lakini leo hii imekuwa fani yenye uwezo wa kumwingizia mtu kipato kikubwa sana,” alisema Tumaini.



Alisema dhumuni la kongamano la siku mbili ni kupambanua fursa zinazopatikana kwenye uchumi wa bluu zinazopatikana baharini ili ziweze kutiwa vvyema na watanzania kwa maeneo ya nchi.



Alisema mpango wa maendeleo wa miaka mitano ulioanza mwaka 2021-2025 umeweka bayana kwamba uchumi wa bluu ni kipaumbele katika shughuli za kuendeleza uchumi wa Tanzania .



Alisema kwenye kongamano hilo pia atahudhuria Waziri wa Uchumi wa Bluu na Uvuvi wa Zanzibar ambaye atakuwa mmoja wa wazungumzzaji wakuu kwenye kjongamano hilo la leo.



“Tutasikia Waziri wetu wa uchumi wa bluu anatuambia nini kuhusu fursa zilizopo kwenye uchumi wetu wa bluu hili ni kongamano la kwanza kabisa la uchumi wa bluu hivyo siy la kukosa na siku ya kufunga tumepata fursa ya kuwa na Waziri wa Elimu, Profesa Adolth Mkenda,” alisema Tumaini

 

 

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post