Dodoma. Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba amesema nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki zimekubaliana kuongeza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 25 hadi asilimia 35 kwenye nywele bandia zinazotambulika kwa Heading 6704.
Dk Mwigulu amesema hayo bungeni leo Jumanne Juni 14, 2022 wakati akiwasilisha makadilio ya mapato na matumizi ya bajeti ya Serikali 2022/23
Amesema “Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki zimekubaliana kuongeza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 25 hadi asilimia 35 kwenye nywele bandia zinazotambulika kwa Heading 6704.
Hatua hii inalenga kulinda wazalishaji wa ndani wa bidhaa hizo, kuongeza ajira pamoja na kuongeza mapato ya Serikali” amesema
Amesema hatua hiyo inalenga kulinda wazalishaji wa ndani wa bidhaa hizo, kuongeza ajira pamoja na kuongeza mapato ya Serikali
"Pamoja na hayo yamefanywa mabadiliko mbalimbali ya sheria kwa kufutwa kifungu cha 5 (1) (l) cha sheria ya chakula, dawa na vipodozi na. 1 ya mwaka 2003 ili jukumu la viwango vya kitaifa libaki kwenye sheria ya viwango na. 2 ya mwaka 2009. Mahitaji ya viwango ya TMDA yatawasilishwa Shirika la Viwango Tanzania.