Wanawake EAC watakiwa kuwania nafasi za uongozi

Anastazia Wambura  akifungua mkutano wa siku tatu wa Afrika wa wanawake ni viongozi kwa niaba ya Spika Dk.Tulia Akson iliyoandaliwa na Taasisi ya Kimataifa inayoshughulikia Demokrasia na uchaguzi (IDEA) kwa kushirikiana na Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA).



 Na Cynthia Mwilolezi, ARUSHA 


WANAWAKE  wa Nchi za Afrika wametakiwa kujitokeza kuwania nafasi mbalimbali za uongozi wa kisiasa, ili kuondoa changamoto zinazowakabili ikiwemo malezi ya watoto .


Aidha, majukumu mengi ya familia na kijamii yanasababisha wengi  wao wenye uwezo wa kuongoza, kutojihusisha na masuala ya siasa badala yake kubaki kulea familia pekee.


Akifungua mkutano wa siku tatu leo jijini hapa  ulioandaliwa na  Taasisi ya Kimataifa ya kusaidia Demokrasia na uchaguzi (IDEA) kwa kushirikiana na Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA),Mbunge Anastazia Wambura kutoka Tanzania kwaniaba ya Spika Dk.Tulia Ackson alisema mkutano huo unalengo  la kujadili changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo wanawake katika masula ya uongozi.


Alisema endapo wanawake wakiwa viongozi wataweza kutatua changamoto mbalimbali za kiongozi,kisiasa na kijamii kwani wao wanabaini changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo ikiwemo malezi ya watoto na ni chombo kikubwa cha amani.


Alitoa rai kwa jamii kuacha kuwaona wanawake kama ni viumbe duni wasioweza kutoa mawazo yao na kujadiliwa lakini uongozi wa kisiasa ni mzuri katika uongozi.


"Lazima sasa tujikwamue wenyewe katika kuwania nafasi mbalimbali za kiungozi na Tanzania tumepiga hatua kubwa Kwa kutoa Rais Mwanamke,Samia Hassan Suluhu na Spika wa Bunge Dk.Tulia Ackson tuongeze idadi ya viongozi wanawake ili tuweza kutatua changamoto mbalimbali "alisema



Pia jamii iache tabia ya  kuona  wanawake hawafai kuongoza, bali wapewe nafasi na mitaala shuleni iwepo kwaaajili ya kuwawezesha wanafunzi wanawake wanajengewa uwezo wa kujiamini na kufanya shughuli mbalimbali ikiwemo kuwania nafasi za kiungozi.


Naye Spika wa Bunge la EALA,Martin Ngoga alisisitiza kuwa haki za wanawake ni haki za binadamu wote, hivyo jamii iwape haki sawa katika kuhakikisha hata wanapotoa michango yao ofisini,kisiasa na kijamii waheshimiwe kwani mwanamke ni kiongozi asiyetetereka.


Naye Fatuma Ndagiza ambaye ni Katibu wa mkutano huo,alisema kuwa mfumo wa vyama vya siasa sio rafiki katika ngazi za uongozi ikiwemo wanawake kutopewa nafasi ya kujadili changamoto zao ikiwemo watoto wa kike hivyo ni vema wanawake wakapambania haki zao ili waweze kuongoza katika nafasi mbalimbali.


This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post