Wazazi watakiwa kulea watoto kwenye maadili

 Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Wazazi na walezi wametakiwa kulea watoto wao katika maadili mazuri yenye kulinda  mila  na desturi ili kuendeleza utamaduni wa kitanzania.

Hayo yameelezwa na baadhi ya wananchi wakazi wa Manispaa ya Shinyanga wakati wakizungumza kwa nyakati tofauti ambapo wamesema wazazi na walezi wanawajibu mkubwa wa kuwafundishwa watoto wao maadili yanayofuata misingi ya Nchi ili kuthibiti wimbi la mmomonyoko wa maadili katika kizazi hiki.

Wamesema kuwekeza kwenye uhifadhi tamaduni, mila na desturi za asili inasaidia kuimarisha utulivu na amani ya Nchi ikiwa ni pamoja na kuzuia migogoro mbalimbali kwenye jamii.

Wananchi hao wamesema wazazi na walezi wanapaswa kuwekeza kwenye malezi na makuzi ya mtoto yanayohifadhi utamaduni wa asili ili kulinda mila na desturi za kitanzania.

Wamesema kwa kufanya hivyo itasaidia watoto kukua katika maadili mema yanayozingatia utamaduni, mila na desturi za makabila yao katika mavazi, heshima na mambo mengine muhimu.

Pia wamesisitiza wazazi na walezi kuwalea watoto katika misingi ya kidini kwa kuhakikisha watoto wanakua katika maadili mazuri yanayozingatia utaratibu wa Nchi ili kutengeneza Taifa bora.

Wametumia nafasi hiyo kuishauri serikali kusimamia sheria na sera zinazomhusu mtoto ili kuhakikisha hazileti athari katika makuzi yake.

Wamepongeza juhudi mbalimbali za serikali zinazofanywa kimkoa na kitaifa kuanza uwekezaji wa makumbusho yanayohifadhi utamaduni wa asili ili kudumisha mila na desturi.

Aidha wananchi hao wamempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuimarisha utamaduni wa Nchi ikiwa ni pamoja na kutangaza utalii ambapo maeneo mbalimbali ya asili katika jamii yanafikiwa.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post