RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AMWAPISHA IGP WAMBURA NA KUMPA MAAGIZO MAZITO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimvalisha Cheo kipya cha Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi (IGP) aliyekuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini (DCI) Camillus Mwongoso Wambura kuwa Mkuu Mpya wa Jeshi la Polisi  katika Hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Jijini Dodoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimwapisha aliyekuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini (DCI) Camillus Mwongoso Wambura kuwa Mkuu Mpya wa Jeshi la Polisi (IGP) katika Hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Jijini Dodoma 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimwapisha aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Simon Nyakoro Sirro kuwa Balozi wa Tanzania Nchini Zimbawe katika Hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Jijini Dodoma 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimwapisha Dkt. Suleiman Haji Suleiman kuwa Balozi katika Hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Jijini Dodoma 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Inspekta Jenerali wa Polisi Camillus Mwongoso Wambura mara baada ya kumwapisha kuwa Mkuu Mpya wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) katika Hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Jijini Dodoma 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Inspekta Jenerali wa Polisi Camillus Mwongoso Wambura na aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Simon Nyakoro Sirro mara baada ya kumwapisha (IGP) Wambura kuwa Mkuu Mpya wa Jeshi la Polisi Ikulu Chamwino Jijini Dodoma ni
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi mbalimbali katika Hafla ya kumwapisha Mkuu mpya wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Camillus Mwongoso Wambura na baadhi ya Mabalozi aliowateua kwenye Hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Jijini Dodoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na CP Mussa Ali Mussa kushoto, Kamishna wa Fedha na Lojistik CP Liberati  Sabas Materu, Kamishna wa Operesheni na Mafunzo Makao Makuu ya Polisi CP Awadhi Juma Haji, na Kamishna wa Polisi Zanzibar Hamad Khamis Hamad katika Hafla ya kumwapisha (IGP) Camillus Mwongoso Wambura Ikulu Chamwino Jijini Dodoma

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ameunda Kamati na Sekretarieti zitakazoshauri namna ya kuleta mabadiliko ya utendaji kazi wenye matokeo bora katika vyombo vya utendaji haki. 


 Rais Samia amesema hayo katika hafla ya uapisho wa Viongozi mbalimbali iliyofanyika Ikulu Chamwino, akieleza kuwa Kamati hiyo itaongozwa na Jaji Mkuu Mstaafu, Mhe. Mohamed Chande Othman.


 Aidha, Rais Samia amesema Kamati hiyo itaanza kulifanyia kazi Jeshi la Polisi na baadae katika majeshi mengine ya ulinzi na vyombo vya utendaji haki. Rais Samia pia amesema Serikali itapitia na kurekebisha miundo, mifumo ya ajira na mafunzo, mifumo ya upandishaji vyeo, madaraka na taaluma za kijeshi.


 Masuala mengine ni kutoa mafunzo kwa majeshi ya ulinzi kuhusu matumizi ya teknolojia ya habari na mawasiliano pamoja na mahusiano ya Jeshi la Polisi na Taasisi zingine ikiwemo Kanuni na Sheria zinazoongoza Taasisi hizo.

Kwa upande mwingine, Rais Samia amelitaka Jeshi la Polisi kufanya kazi kwa ufanisi, na kuimarisha usalama wa raia na mali zao na kuzingatia haki za binadamu

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post