Serikali Yatoa Agizo Kukamilisha Ujenzi wa Kituo cha Afya Kibaoni

Serikali Yatoa Agizo Kukamilisha Ujenzi wa Kituo cha Afya Kibaoni


 Na Fred Kibano, Mpimbwe Katavi 

 Serikali imeagiza kukamilishwa kwa ujenzi wa kituo cha Afya kibaoni kilichopo Halmashauri ya Wilaya Mpimbwe ifikapo mwezi Septamba ili wananchi wa eneo hilo wapate huduma za afya karibu na makazi yao. 


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango ametoa agizo hilo baada ya kufanya ziara ya kikazi wilayani humo na kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa kituo hicho hivi leo na kujionea hatua ya ujenzi iliyofikiwa na ndipo aliwataka watendaji kuongeza kasi ya ujenzi wa kituo hicho. 


 “dhamira ni ile ile, Mama Samia anachotaka ni kusogeza huduma karibu na wananchi, lakini nasisitiza tena madaktari, wahududumu wote wa afya mkawahudumie wananchi hawa kwa upendo, tumekubaliana na Naibu Waziri TAMISEMI mwezi wa tisa kukamilisha ile kazi ili tarehe 1 Oktoba mwaka huu kituo kianze kuhudumia wananchi” alisema Mhe. Dkt. Mpango 


Akitoa salamu za mkoa wa Katavi, Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko amesema Ofisi yake inaahidi kuendelea kusimamia fedha za miradi ya Sekta zote kwani fedha za Tozo ya miamala ya simu pekee mkoa ulipokea shilingi Bilioni 13.08 ambazo pia katika Sekta ya Afya zimejenga vituo vya afya sita vilivyopata shilingi milioni 500 kila kimoja ambavyo vinaendelea kukamilika. 


 Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Dkt. Festo Dugange amesema amepokea maelekezo ya Serikali kuhakikisha Kituo cha Afya Kibaoni kinakamilika mwishoni mwa mwezi wa tisa ili kianze kutoa huduma na kuondoa kero kwa wananchi kwenda kutibiwa umbali mrefu. 


 

“Mhe. Makamu wa Rais, tumepokea maelekezo yako kwamba ifikapo tarehe 30 mwezi wa tisa mwaka huu kituo kile kiwe kimekamilika, naomba nikuhakikishie kuwa Ofisi ya Rais TAMISEMI tutahakikisha tunashirikiana na Mkoa na Halmashauri kuhakikisha kituo kile kinakamilika ifikapo tarehe 30 mwezi wa tisa” alisema Mhe. Dkt. Dugange. 


 Mbunge wa Jimbo la Kivuu Geophrey Pinda 

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post