Tanzania kuwa mwenyeji Mkutano nchi zinazozalisha Almasi Afrika

 Na Veronica Mheta, Arusha



TANZANIA kuwa mwenyekiti wa mkutano wa tatu wa dharura wa Baraza la Mawaziri wa nchi zinazozalisha Almasi Afrika (ADBA) ambao utaidhinisha katiba,kanuni na miongozo ya umoja huo


Mkutano huo unaoendela leo Jijini Arusha utateua viongozi watatu wa sekretarieti ambao ni katibu Mtendaji na manaibu wake wawili.


 Waziri wa Madini ,Doto Biteko,amesema  mkutano huo  wa tatu wa dharura wa Baraza  la Mawaziri wa Jumuiya ya nchi za Afrika zinazozalisha Almasi (ADPA)  kwa mujibu wa utaratibu ulianza  Aprili 7 mwaka 2022  kwa kamati ya wataalamu kuchambua na kujadili nyaraka mbalimbali zinazohusiana na mapitio na marekebisho ya nyaraka zinazosimamia ADPA  


Biteko anasema lengo kubwa la kuunda ADPA  ni kuzipatia nchi zinazozalisha Almasi Afrika Jukwaa la kuzikutanisha nchi zote za Afrika katika kusudi moja la kuhakikisha rasilimali za madini hayo zinanufaisha  nchi wanachama.



"Tanzania ilichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri la ADPA  mwaka 2021 kwa kipindi cha miaka miwili,hivyo tunatarajia kukabidhi uenyekiti wetu kwa Jamuhuri ya Zimbabwe Machi mwaka 2023"


Amesema katika kipindi cha Tanzania kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, imekuwa ni heshima kubwa kwao kwa kuwajibika, kwa ajili ya kuwezesha maendeleo ya nchi zao hususan katika usimamizi wa madini ya almasi 


This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post