Raila ashindwa Urais Kenya,Mahakama yampitisha Ruto

Mahakama ya juu imeidhinisha uchaguzi wa William Ruto kuwa Rais mteule wa Kenya baada ya kesi iliyowasilishwa na mpinzani wake mkuu katika uchaguzi Raila Odinga kukosa ushahidi wa kutosha.


Wakitoa uamuzi wao wa pamoja, majaji hao walioongozwa na haki mkuu Martha Lione walisema kwamba ushahidi uliotolewa na mlalamishi Raila Odinga ya ulikuwa ujaa uvumi na porojo.


Akiangazia maswala tisa ya kesi hiyo, Jaji Martha Koome amesema kuwa mshindi wa uchaguzi huo William Ruto alifanikiwa kupita kikwazo cha kura asilimia 50 na moja ya kikatiba.


Akitangaza matokeo hayo , mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) Wafula Chebukati, alimtangaza Dkt Ruto kuwa Rais mteule baada ya kupata kura milioni 7,176,141 (asilimia 50.49) dhidi ya milioni 6,942,930 za Bw Odinga (asilimia 48.85) )Prof George Wajackoyah wa Roots Party alifanikiwa kura 61,969 (asilimia 0.44) huku David Mwaure Waihiga wa Agano Party akiibuka wa nne kwa kura 31,987 (asilimia 0.23).


Akitoa uamuzi huo jaji mkuu Martha Koome alisema kwamba kura zilizokataliwa haziwezi kujumlishwa katika hesabu ya kumtafuta aliyeibuka mshindi.


Bi Martha Koome alisema kwamba mbinu iliotumika na tume ya uchaguzi kupata asilimia 64.4 ya wapiga kura ilikuwa sahihi.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post