IDARA YA WANAWAKE KANISA LA AICT (TAIFA) YAANZA SEMINA SHINYANGA ASKOFU BUGOTA ASISITIZA USHIRIKIANO

Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Makamu wa Askofu Mkuu wa AICT Askofu Zakayo Bugota ambaye pia ni Askofu wa kanisa la Africa Inland Church Tanzania, Dayosisi ya Shinyanga leo amefungua semina ya idara ya wanawake wa AICT ambayo itafanyika kwa siku tatu katika ukumbi wa chuo cha ualimu SHYCOM mjini Shinyanga.

Askofu Bugota ametumia nafasi hiyo kuwakumbusha kuendelea kushirikiana na serikali pamoja na wadau wengine katika juhudi za kukemea mmomonyoko wa maadili, tabia na destori kandamizi pamoja na migogoro ya ndoa na familia.

Amesema ipo haja ya kuendelea kushirikiana ili kuhakikisha wanapaza sauti ya pamoja kukemea tabia zinazokwenda kinyume na maadili ikiwemo mavazi yasiyo na staha.

“Zipo changamoto zinazohitaji mkakati wa pamoja moja wapo ya kazi kubwa ambayo idara ya wanawake iko mbele yenu ni mmomonyoko wa maadili ambayo inahitaji mshikamano wa pamoja katika kuishughulikia, tunaishukuru serikali kwa kuendelea kutoa wito kwa wadau kushirikiana katika kukemea matendo yanayoleta aibu kwa jamii yetu”.

“Wanawake waumini wa kanisa la AICT tuwe mstari wa mbele kukemea na kutoa elimu za kubadili tabia tuzikatae tabia kama za ushoga, kutoheshimiana, kuzoelea mitandao michafu, uvutaji na utumiaji wa madawa ya kulevya, ulevi na tabia zingine kama hizo, neno la Mungu linaagiza ‘wala msifuatishe namna ya Dunia hii, bali mgeuzwa kwa kufanywa upya nia zenu mpate kujua kakika mapenzi ya Mungu yalivyomema ya kupendeza na ukamilifu”.amesema Askofu Bugota

“Kuna migogoro ya ndoa na familia hii ni mojawapo ya chanzo cha ongezeko la watoto wa mitaani n ahata mauaji ya kutisha tunayoyaona katika jamii na kundi kubwa la waathirika ni wanawake na watoto lakizi zipo tabia na desturi kandamizi tuendelee kuelimisha kanisa ili waumi wetu wawe mstari wa mbele katika mabadiliko haya”.amesema Askofu Bugota

Askofu Bugota ametumia nafasi hiyo kuwaomba wanawake hao kutumia fursa mbalimbali zinazojitokeza ikiwemo zile za kiuchumi ili kupata vyanzo vya mapato vitakavyowawezesha kujikwamua kimaisha.

“Zipo rasilimali tulizopewa na Mungu tuzitumie kuboresha maisha ya watu kimsingi mwanamke akiimarika kiuchumi familia na kanisa litaimarika pia kiuchumi tuweke jitihada katika kulinda rasilimali zetu hii ikiwa ni pamoja na kupanda miti na kuepuka kupanda miti ovyo lakini pia kuharibu vyanzo vya maji tuendeleze kauli mbiu ya Tanzania Nchi ya kijani na mtu na mti”.

“Jitihada za mafundisho ya neno la Mungu kuhusu Imani na wokovu zipewe kipaumbele katika kutatua changamoto ya uchanga wa maisha ya kiroho lakini pia upo uchumi duni kwa wanawake katika kanisa na jamii tuweke jitihada za makusudi za kuwasaidia waumini kuzibaini rasilimali zilizopo na kuzitumia ili kuondokana na hali duni ya maisha idara ya wanawake iongeze mafundisho ya ujasiliamali kwa wanawake na kuwasaidia kuunda vikundi vya kiuchumi ili kutoa fursa kwa wanawake kupata mikopo ya kifedha ya serikali au taasisi za kifedha”.amesema Askofu Bugota

Mwenyekiti wa idara ya wanawake kanisa la AICT Bi. Martha Misoji amemshukuru Askofu Bugota ambapo ameahidi kuwa idara hiyo itaendelea na jitihada mbalimbali za kuwaimarisha wanawake wa kanisa hili.

Amesema Dayosisi zinazoshiriki semina hiyo ni Dayosisi ya Pwani, Dayosisi ya Mwanza, Dayosisi ya Geita, Mara, ukelewe pamoja na Dayosisi ya kati.

Mwenyekiti wa CCT Bi. Naila Mayala naye ametumia nafasi hiyo kuwasisitiza washiriki wa semina hiyo kuwa mabalozi wazuri kwa wengine.

Aidha Bi. Naila amewaomba wanawake hao kuendelea kushirikiana katika kutokomeza Mmomonyoko wa maadili na kutoa elimu juu ya malezi na makuzi ya watoto.

Wanawake wa kanisa la AICT katika Dayosisi saba leo Jumatano Juni 14,2023 wameanza semina ya siku tatu yenye lengo la kuwaimarisha kimwili na kiroho kukemea mambo maovu ikiwa ni maandalizi ya kuelekea wiki ya wanawake inayofanyika kila Mwaka mwezi Septemba.

Makamu wa Askofu Mkuu wa AICT Askofu Zakayo Bugota ambaye pia ni Askofu wa kanisa la Africa Inland Church Tanzania, Dayosisi ya Shinyanga akifungua semina ya idara ya wanawake katika ukumbi wa mikutano chuo cha ualimu SHYCOM mjini Shinyanga.

Makamu wa Askofu Mkuu wa AICT Askofu Zakayo Bugota ambaye pia ni Askofu wa kanisa la Africa Inland Church Tanzania, Dayosisi ya Shinyanga akizungumza kwenye hiyo katika ukumbi wa chuo cha ualimu SHYCOM mjini Shinyanga.

Mwenyekiti wa idara ya wanawake kanisa la AICT Bi. Martha Misoji akizungumza kwenye semina hiyo leo Jumatano Juni 14,2023 katika ukumbi wa mikutano chuo cha SHYCOM mjini Shinyanga.

 

Semina ya idara ya wanawake wa kanisa la AICT ikiendelea katika ukumbi wa mikutano chuo cha ualimu SHYCOM mjini Shinyanga.



This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post