Na Mapuli Misalaba, Shinyanga
Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga limesema kesi
mbalimbali zimefanikiwa mahakamani ambapo watuhumiwa kadhaa wa makosa ya
kiharifu wamehukumiwa adhabu kulingana na makosa yao.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo kwa vyombo vya
habari na kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga kamishna msaidizi wa
Polisi Janeth Magomi katika kipindi cha mwezi mmoja kuanzia mwezi Julai hadi
Juni 21,2023.
Kamanda Magomi amesema miongoni mwa kesi zilizopata
mafanikio ni pamoja na kesi moja ya mauaji mtuhumiwa amehukumiwa adhabu ya kunyongwa
hadi kufa, kesi moja ya kujaribu kubaka imehukumiwa kifungo cha miaka 20 jela,
kesi mbili za kubaka zimehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela kila moja, kesi
moja ya kumpa mimba mwanafunzi mtuhumiwa amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela
pamoja na kesi moja ya kutorosha mwanafunzi imehukumiwa kwa kifungo cha miaka
30 jela.
Ametaja kesi zingine kuwa ni pamoja na kujeruhi ambayo
imehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela, kujifanya mtumishi wa serikali
imehukumiwa miaka miwili(2) jela, kuvunja nyumba usiki imehukumiwa miaka mitano
(5) jela na wizi wa gari kesi hiyo imehukumiwa miaka mitatu( 3) jela.
Katika kipindi hicho pia jeshi la polisi Mkoa wa
Shinyanga limefanya misako na doria mbalimbali ambapo limefanikiwa kukamata
vitu na vielelezo mbalimbali ikiwemo silaha aina ya Chinese pistol yenye namba
071T4823 ikiwa na risasi tano(5), pikipiki nne(4), Baskeli mbili(2), mafuta ya
diesel lita 60, petrol lita 20, dawa za
kulevya aina ya bangi kilo 60 na gramu 540, mitungi bunda 58, Heroine kete 166,
Televisheni mbili(2), Gogoro moja, Subwoofer moja na CPU moja.
“Jumla ya
watuhumiwa 19 tumewashikilia na wengine kati yao wakiwa nje kwa dhamana kwa
kuhusika na makossa mbalimbali yaliyotajwa hapo juu”amesema kamanda Magomi
Amesema katika upande wa usalama barabarani jumla ya makosa
3,352 yamekamatwa na kulipiwa faini, madereva wawili wa mabasi wamefungiwa
leseni zao kwa kwa kukiuka taratibu za usalama barabarani ambapo kamanda huyo
amewataka watumiaji wa barabara kufuata sheria za usalama barabani ili kuepuka
ajali.
Aidha Makanda Magomi amezishukuru na kuzipongeza idara za mahakama na mwanasheria wa serikali kwa kuhakikisha adhabu kali zinatolewa kwa wale wanaopatikana na hatia kwa vitendo mbalimbali vya kiharifu.
Kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga kamishna
msaidizi wa Polisi Janeth Magomi akizungumza na waandishi wa habari leo
Jumatano Juni 21,2023
Kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga kamishna
msaidizi wa Polisi Janeth Magomi akionesha silaha aina ya Chinese Pistol ikiwa
na risasi tano leo Jumatano Juni 21,2023
Kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga kamishna
msaidizi wa Polisi Janeth Magomi akionesha bangi iliyokamatwa.