MGEJA AWAOMBA WATANZANIA KUUNGA MKONO UWEKEZAJI WA BANDARI NA KUPUUZA UPOTOSHWAJI NA UPANDIKIZAJI CHUKI

 Suzy Luhende 


 Mwenyekiti  wa Taasisi ya Mtanzania Mzalendo Foundation Hamis Mgeja, amewaomba watanzani wapuuze propaganganda za upotoshwaji na  upandikizaji wa chuki za kuleta udini na ukabila ambayo hayana afya kwa watanzania yanaweza kusababisha kuligawa Taifa, hivyo kuwaomba watanzania waunge mkono uwekezaji wa bandari.

Hayo ameyasema jana wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini Shinyanga,  ambapo amesema baadhi ya watu wamekuwa wakipotosha jamii juu ya mkataba wa uwekezaji wa bandari na kuleta ukabila na udini hali ambayo inaweza kusababisha machafuko.

Amesema yeye kama mwenyekiti wa Taasisi ya Tanzania Mzakendo Foundation inayojihusisha  na masuala ya haki, demokrasia na utawala bora, amelaani kitendo cha baadhi ya watu kupitia mitandao ya kijamii kupotosha Umma suala la Mkataba wa uwekezaji Bandari ya Dar es salaam pamoja na kupandikiza chuki za udini na ukabila.

"Sisi  kama Taasisi ya Mtanzania Mzalendo Foundation, tumefanya uchambuzi wa kina pamoja na kufuatilia mijadala mbalimbali ikiwamo kusikiliza bunge, na tumejiridhisha pasipo shaka yoyote, kwamba mpango wa Serikali kuhusu uwekezaji wa Bandari ya Dar es salaam ni mzuri na tumeunga mkono asilimia 100 kwa maslahi mapana ya Taifa, na tumelaani upotoshaji na upandikizaji wa chuki,"amesema Mgeja.

“Tunaimani na Serikali haiwezi kupotosha umma wala kuuza maslahi ya nchi, tumeona Bunge limeridhia suala hili, na sisi kama Watanzania tumeona jambo hili tulizungumze na kumuunga mkono Rais wetu Samia juu ya uwekezaji wa Bandari ya Dar es salaam baina ya Tanzania na Falme za  Dubai,”ameongeza.

Amesema suala la kubinafsisha hali jaanza katika awamu ya Sita, na pale panapo onekana hakuna ufanisi, ni vyema wakatafutwa wawekezaji ili kuongeza ufanisi na kupata mapato mengi kwa mashali ya Taifa, na kuomba hata Bandari ya Bagamoyo, Tanga na Mtwara napo patafutwe wawekezaji.

“kuoitia taasisi hii nimuomba Rais azibe masikio, hata kwenye Filamu ya Royal Tour napo kulikuwa na maneno mengi, leo tumeona faida yake fedha za kigeni zimeongezeka kutokana na Sekta ya Utalii, na hili jambo la uwekezaji wa Bandari mafanikio yake tutayaona na wanaopinga watakuja kusema tulichelewa,” amesema Mgeja.

Baadhi ya wananchi wa manispaa ya Shinyanga akiwemo Thomas Tungu amesema kwa watu ambao bado wanapinga uwekezaji huo wa Bandari ya Dar es salaam, waje sasa na mbadala kwamba wao wanaweza kufanyanini, au kama hawakubaliani mtu mwenye dini flani au kabila flani waeleze wao wanataka mtu mwenye dini gani au kabila gani, na kusema kwamba wasiwe Mahodari wa upotoshaji bali waje na mawazo ya kujenga nchi na siyo kuleta chuki za kidini.

“Bandari ndiyo Sekta mama, mapato ambayo yanaweza kupatikana katika uwekezaji huu, tangia tupate uhuru hayataweza kupatikana kama yatakavyo patikana katika mpango huu, hivyo tuiunge mkono Serikali yetu”amesema Anastanzia Jeremia mkazi wa Manispaa ya Shinyanga.

Hata hivyo hivi karibuni Wazee, Viongozi wa Dini na Machifu mkoani Shinyanga, nao walitoa tamko la kumuunga mkono Rais Samia juu ya Mkataba wa uwekezaji wa Bandari na kulaani juu ya upotoshaji kwa baadhi ya watu ambao hawana nia njema na Taifa kusongambele kimaendeleo.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post